Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Zerbi: Spurs subirini pira biriani

SPURS Pict

Muktasari:

  • De Zerbi amekiri kuwa kazi iliyo mbele yake ni kubwa, lakini amesisitiza kwamba ana imani na ubora wa wachezaji wake na atafanya kila awezalo kuisaidia timu kurejea kwenye njia ya ushindi.

LONDON, ENGLAND: Kocha mpya wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, ameahidi kuirejeshea hadhi klabu hiyo na kuwapa mashabiki aina ya soka la kuvutia lililokuwa likichezwa chini ya aliyekuwa kocha wao, Ange Postecoglou.

De Zerbi, ambaye mchezo wake wa kwanza kama kocha wa Spurs utakuwa wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland leo saa 10:00 jioni, amesaini mkataba wa miaka mitano bila kuwapo kwa kipengele cha kuondoka endapo timu hiyo itashuka daraja.

Kocha huyo wa Kiitaliano amesema ana mpango wa kukaa muda mrefu na kwamba malengo yake ni kuirudisha Spurs katika nafasi za juu kwenye ligi hiyo, ingawa kwa sasa hafikirii kuhusu mataji bali kuijenga kuwa imara na yenye ushindani.

De Zerbi ameeleza kuwa falsafa yake ya soka ni kucheza kwa kushambulia na kumiliki mpira, akisisitiza kuwa angependa kuona tena kiwango kilichowavutia mashabiki wakati wa Postecoglou.

Amesema msimu wake wa pili akiwa kocha wa Brighton, Spurs ilionyesha soka la kuvutia, na anaamini wachezaji waliopo sasa wana uwezo wa kuendeleza mtindo huo akiwataja kwa majina Pedro Porro, Destiny Udogie, Micky van de Ven na Cristian Romero kama mfano wa nyota wanaoweza kutekeleza mpango wake wa kucheza kwa kasi na kushambulia zaidi, huku akisisitiza kuwa “DNA” ya klabu ni kutafuta mabao.

Hata hivyo, kipaumbele cha haraka kwa sasa ni kuinusuru timu isishuke daraja. Tottenham haijashinda mechi 13 mfululizo za ligi tangu Desemba, 2025 ikiwa tayari imebadili makocha mara mbili msimu huu baada ya kuachana na Thomas Frank mwezi Februari, kisha Igor Tudor wiki chache baadaye.

De Zerbi amekiri kuwa kazi iliyo mbele yake ni kubwa, lakini amesisitiza kwamba ana imani na ubora wa wachezaji wake na atafanya kila awezalo kuisaidia timu kurejea kwenye njia ya ushindi.