Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Zerbi aipa sharti moja Tottenham Hotspur

DE ZEBRI Pict

Muktasari:

  • Tudor alipewa mkataba wa kuifundisha Spurs hadi mwisho wa msimu ambapo kama akifanya vizuri ataendelea na akifanya vibaya atatafutwa kocha mwingine wa kudumu. De Zerbi anaonekana kuwa mmoja wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Spurs.

LONDON, ENGLAND: Inaelezwa kocha raia wa Italia Roberto De Zerbi yuko tayari kuchukua kazi ya kuifundisha Tottenham Hotspur kwa msimu ujao lakini kwa sharti la timu hiyo kwanza kubakia Ligi Kuu msimu huu.

Spurs imekuwa katika hali mbaya sana msimu huu hadi ikafikia kumtimua kocha Thomas Frank mwezi uliopita baada ya kujikuta wakikaribia kushuka daraja. Hata hivyo, matokeo na kiwango cha timu havijaimarika chini ya kocha mpya wa muda Igor Tudor huku klabu hiyo sasa ikiwa na tofauti ya pointi moja tu juu ya timu tatu za mwisho zilizo katika hatari ya kushuka daraja.

Tudor alipewa mkataba wa kuifundisha Spurs hadi mwisho wa msimu ambapo kama akifanya vizuri ataendelea na akifanya vibaya atatafutwa kocha mwingine wa kudumu. De Zerbi anaonekana kuwa mmoja wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Spurs.

Gazeti la Telegraph limeripoti kuwa De Zerbi ambaye kwa sasa hana timu baada ya kuondoka Marseille mwezi uliopita ameshazungumza na Tottenham na anatajwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa mbali ya kocha wa zamani wa klabu hiyo, Mauricio Pochettino.

Kwa sasa De Zerbi yuko tayari kuinoa Tottenham lakini msimamo huo unaweza kubadilika ikiwa matokeo yataisababishia kushuka daraja.

De Zerbi alijizolea sifa kubwa EPL kwa kazi nzuri aliyofanya akiwa kocha wa Brighton aliyoifundisha kwa miaka miwili.