Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunha ajiweka hatarini kufungiwa

CUBHA Pict

Muktasari:

  • Baada ya kufunga bao hilo, Cunha alikimbia kusherehekea na kuzingirwa na wachezaji wenzake, kabla ya kuangalia moja kwa moja kwenye kamera na kusikika akisema maneno ya matusi. Bao hilo lilitosha kuifanya Man United kudumisha rekodi ya ushindi wa asilimia 100 chini ya kocha wa muda, Michael Carrick.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa Manchester United, Matheus Cunha, huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa baada ya kutumia maneno yasiyofaa wakati aliposhangilia bao lake. Mshambuliaji huyo alifunga bao la kushangaza lililoipa Man United ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates.

Baada ya kufunga bao hilo, Cunha alikimbia kusherehekea na kuzingirwa na wachezaji wenzake, kabla ya kuangalia moja kwa moja kwenye kamera na kusikika akisema maneno ya matusi. Bao hilo lilitosha kuifanya Man United kudumisha rekodi ya ushindi wa asilimia 100 chini ya kocha wa muda, Michael Carrick.

Dakika chache baada ya tukio hilo, mtangazaji wa Sky Sports, Peter Drury, aliomba radhi akisema: “Ikiwa mlisikia lugha isiyofaa wakati wa sherehe za bao, tunaomba radhi.”

Chama cha Soka England (FA) kimekuwa kikichukulia kwa uzito mkubwa wachezaji wanaotukana moja kwa moja mbele ya kamera. Mwaka 2011, gwiji wa Man United, Wayne Rooney, alifungiwa michezo miwili baada ya kufanya hivyo katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham. Hivyo basi, Cunha yuko katika hatari ya kuadhibiwa kwa njia hiyo hiyo.

Sheria za Mchezo za IFAB zinasema wazi wachezaji hawaruhusiwi kutumia lugha au vitendo vya kuudhi, kudhalilisha au matusi. Endapo mwamuzi atasikia, mchezaji anaweza kuonyeshwa kadi nyekundu.

Hata hivyo, kama mwamuzi hajasikia, FA ina mamlaka ya kuchukua hatua za baadaye, hasa pale tukio linapokuwa limerekodiwa na kurushwa kwa hadhira kubwa. FA hutazama matusi yanayosemwa moja kwa moja mbele ya kamera kama kitendo cha wazi na cha makusudi kinachoharibu taswira ya mchezo.

Bado haijajulikana kama FA itachukua hatua dhidi ya Cunha na endapo itafanya hivyo, itachukua muda gani kufikia uamuzi na adhabu husika.