Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunha ajifunza mapigano kudhibiti hasira uwanjani

CUNHA Pict

Muktasari:

  • Mkali huyo mpya wa Man United anafundishwa mapigano hayo na bingwa wa zamani wa dunia na Ulaya wa Jiu Jitsu, Lucio Rodrigues.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa Manchester United, Matheus Cunha amekuza makali yake uwanjani kwa kujifunza sanaa ya mapigano ya Kibrazili, Jiu Jitsu.

Mkali huyo mpya wa Man United anafundishwa mapigano hayo na bingwa wa zamani wa dunia na Ulaya wa Jiu Jitsu, Lucio Rodrigues.

Cunha, 26, alianza mazoezi na Lucio, anayejulikana kwa jina la utani Lizard, Desemba mwaka jana na mazoezi hayo yanazingatia vipindi vya kiufundi na vyenye udhibiti, ili kusaidia utendaji wake, usawa na uhamasishaji.

Lucio, 45, mwenye mkanda mweusi wa Jiu Jitsu, hupanga mazoezi ya Cunha kwa kuweka mkazo kwenye usalama na kuzuia majeraha ili asipate matatizo na mabosi wa Man United.

Jiu Jitsu inatambuliwa kwa upana kama sanaa ya mapigano yenye nidhamu na njia ya kudhibiti hisia na hasira kwa mpangilio maalum.

Katika chapisho la Instagram, Lucio, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, uzito wa juu (super-heavyweight) na mpiganaji wa zamani wa MMA,  amesema ni "heshima ya kweli” kushiriki maarifa yake na Cunha, ambaye alimwelezea kama “mfano wa kuigwa wa kweli ndani na nje ya uwanja wa mazoezi.”

Aliongeza: “Kuwa na imani yake na imani ya familia yake, kufanya mazoezi nami ni jambo ninalolithamini na kujivunia.”

Cunha pia alichapisha video fupi akipokea mkanda kutoka kwa Lucio wakati wa mazoezi. Cunha amekuwa na mafanikio makubwa Man United tangu kuwasili kwake majira ya joto yaliyopita.

Lakini katika klabu yake ya zamani ya Wolves, alipata sifa ya kuwa na uchokozi usiodhibitiwa uwanjani baada ya matukio kadhaa ya vurugu. Alishtakiwa na FA, Machi mwaka jana baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipigo cha mikwaju ya penalti kwenye Kombe la FA dhidi ya Bournemouth. Cunha alishtakiwa kwa “kutenda kwa njia isiyofaa” baada ya kutolewa nje kwa kugombana na beki wa Bournemouth, Milos Kerkez, dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza.

Alimshambulia Kerkez mara tatu, akipigana naye na kumpiga teke kabla ya kujaribu kumpiga kichwa wakati beki huyo wa kimataifa wa Hungary aliposimama tena. FA ilimpa adhabu ya kufungiwa mechi nne na faini ya Pauni 50,000. Na Desemba 2024, Cunha alifungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya Pauni 80,000 baada ya kugombana na mfanyakazi wa usalama wa Ipswich Town na kumvua miwani yake kufuatia ushindi wa 2-1 wa wageni hao katika uwanja wa Molineux. Kudhibiti hasira hizo, Cunha ameamua kufanya mafunzo ya Jiu Jitsu.