Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Courtois majanga tena, kukaa nje miezi miwili

Muktasari:

  • Courtois mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akifanya mazoezi ya kurejea tena katika hali ya utimamu wa mwili baada ya kuwa nje akiuguza majeraha ya goti aliyoyapata mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois atakuwa nje kwa miezi miwili baada ya kupata majeraha akiwa mazoezini leo mchana.

Courtois mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akifanya mazoezi ya kurejea tena katika hali ya utimamu wa mwili baada ya kuwa nje akiuguza majeraha ya goti aliyoyapata mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Inalezwa kuwa vipimo vya awali vimeonyesha 'meniscus' yake katika goti la kulia imejeruhiwa na  atalazimika kufanyiwa upasuaji tena ili awe sawa.

Upasuaji huo mpya unakadiriwa kuwa utamuweka tena nje kwa miezi miwili hadi mitatu hali inayoweza kumsababishia kukosa michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza Juni 14,  mwaka huu.

Ili kuziba nafasi yake baada ya kuumia, mabosi wa Real Madri walimsajili Kepa Arrizabalaga kwa mkopo kutoka Chelsea. Mbali ya Kepa, pia Madrid imekuwa ikimtumia kipa wao raia wa Ukraine Andriy Lunin.