Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyopitia Suarez Uruguay ikilazimishwa sare na Cape Verde

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 ya kundi  H, kwenye fainali za Kombe la Dunia, nyota huyo wa zamani wa Liverpool na Barcelona anayekipiga kwa sasa Inter Miami, alionekana akiwa na wasiwasi huku akiwa ameshika kichwa na kukata tamaa wakati mechi ikiendelea kutokana na matukio ndani ya uwanja, ikiwamo kushangilia bao la kiusawazisha la Uruguay.

Nyota wa zamani wa Uruguay, Luis Suarez alijikuta katika wakati mgumu akiitazama timu yake ya taifa ikicheza dhidi ya Cape Verde.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 ya kundi  H, kwenye fainali za Kombe la Dunia, nyota huyo wa zamani wa Liverpool na Barcelona anayekipiga kwa sasa Inter Miami, alionekana akiwa na wasiwasi huku akiwa ameshika kichwa na kukata tamaa wakati mechi ikiendelea kutokana na matukio ndani ya uwanja, ikiwamo kushangilia bao la kiusawazisha la Uruguay.

Cape Verde ndiyo ilianza kupata bao dakika ya 21 la Kevin Pina, kabla ya Uruguay kusawazisha dakika ya 44 kupitia Maxi Araujo na dakika moja Agustin Canobbio kufunga la pili na ubao kusoma 2-1 hadi kipindi cha kwanza kilipotamatika.

Baada ya matokeo hayo ya kipindi cha kwanza, wengi walidhani uruguay ya Kocha Marcelo Bielsa ingeondoka na ushindi kwa kuongeza mabao mengine, lakini haikuwa hivyo na Cape Verde ilipambana na kutengeneza hatari nyingi langoni mwa Uruguay, kabla ya kusawazisha kwa bao la nyota wa Maccabi Tel Aviv, Helio Varela dakika ya 61.

Suarez katika historia ya Kombe la Dunia anakumbukwa kwa mengi lakini kubwa zaidi ni lile la mwaka 2010, alipojifanya kipa na kudaka mpira dakika za mwisho za mechi dhidi ya Ghana katika harakati za kuoa hatari.

Katika mechi hiyo, Suares alilimwa kadi nyekundu na Ghana kuzawadiwa penalti ambayo hata hivyo nahodha wao, Gyan Asamoh alikosa na kuibua shangwe kwa nyota huyo ambaye wakati huo alikuwa akielekea vyumbani kuanza kuitumikia adhabu yake ya kukosa mechi tatu zinazofuata.