Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Palmer aipa pigo jingine Chelsea

Muktasari:

  • Kocha wa The Blues, Enzo Maresca amethibitisha kwamba kiungo huyo mshambuliaji atakosa walau mechi tatu zijazo za timu hiyo, ikiwamo ile ya Jumamosi jioni dhidi ya Burnley.

LONDON, ENGLAND: COLE Palmer ameipa pigo jingine Chelsea kutokana na kuumia kidole wakati akiwa nyumbani.

Kocha wa The Blues, Enzo Maresca amethibitisha kwamba kiungo huyo mshambuliaji atakosa walau mechi tatu zijazo za timu hiyo, ikiwamo ile ya Jumamosi jioni dhidi ya Burnley.

Kocha Maresca, 45, alisema staa huyo alipata ajali nyumbani kwake na kuumia kidole.

Hiyo ina maana, Chelsea haitakuwa na huduma yake katika mechi tatu dhidi ya Burnley, Barcelona na Arsenal.

Mara ya mwisho Palmer kuichezea Chelsea ilikuwa Septemba. Alitolewa mapema katika kipindi cha kwanza uwanjani Old Trafford katika mechi dhidi ya Manchester United.

Kilichokuwa kikimweka nje Palmer kabla ya kuumia kidole ilikuwa maumivu ya misuli ya nyonga. Kiungo huyo alikuwa akimpa uhakika Maresca wa kurejea uwanjani mwezi huu.

Hata hivyo, Palmer amejiumiza na mlango kidole kwenye mguu wa kushoto na kuumia na hilo limempa wakati mgumu kocha wa miamba hiyo ya Stamford Bridge.

Maresca alisema: “Palmer hatakuwapo, bila shaka kwenye mechi dhidi ya Barcelona na Arsenal. Kwa bahati mbaya alijiumiza kidole cha mguu. Ndiyo hivyo, hatakuwapo hata wiki ijayo.”

Chelsea itafanya kila inachoweza kuhakikisha mchezaji huyo anapona haraka na kurudi mazozini. Kukosekana kwa Palmer kwenye fowadi ya Chelsea kubainisha pengo kubwa huku wachezaji Joao Pedro, Enzo Fernandez na Estevao wakishindwa kuonyesha kuziba pengo hilo.


MECHI TANO ZIJAZO ZA CHELSEA

-Novemba 22 vs Burnley (ugenini)

-Novemba 25 vs Barcelona (nyumbani)

-Novemba 30 vs Arsenal (nyumbani)

-Desemba 3 vs Leeds United (ugenini)

-Desemba 6 vs Bournemouth (ugenini)