Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cole Palmer achoshwa na maisha ya Chelsea

PALMER Pict

Muktasari:

  • Klabu kubwa England, Manchester United, Real Madrid, na Bayern Munich zinafuatilia kwa karibu hali ya nyota huyo wa England, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni 150 milioni.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Chelsea, Cole Palmer, anadaiwa kukata tamaa juu ya maisha yake katika viunga vya Stamford Bridge na anaonekana kuwa tayari kuondoka mwisho wa msimu huu.

Klabu kubwa England, Manchester United, Real Madrid, na Bayern Munich zinafuatilia kwa karibu hali ya nyota huyo wa England, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni 150 milioni.

Palmer, mwenye umri wa miaka 23, anaripotiwa kukerwa na mabadiliko ya mbinu za uchezaji ndani ya Chelsea, akiamini zimempunguzia nafasi ya kufanya uamuzi uwanjani. Pia amechukizwa na kuondoka kwa mshambuliaji Nicolas Jackson, ambaye kwa sasa yupo Bayern Munich kwa mkopo wa msimu mzima.

Uwepo wa Jackson, ambaye ana kasi na mikimbio bora kabisa ulikuwa ukimsaidia kwa Palmer ambaye msimu uliopita alifunga mabao 18 na kutoa pasi 14 za mabao.

Mshambuliaji huyo wa Senegal aliondoka Septemba, mwaka jana, baada ya Chelsea kuwasajili Joao Pedro na Liam Delap. Msimu huu, Palmer, aliyewahi kucheza Manchester City amekuwa na kiwango cha kawaida huku akikumbwa na majeraha ya nyonga na kidole cha mguu.

Chini ya kocha Liam Rosenior, Chelsea ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England na wako hatarini kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Kukosa nafasi hiyo kunaweza kuongeza uwezekano wa Palmer kuondoka na kutua Manchester United, inayotajwa kuwa timu aliyokuwa akiishabikia utotoni.

Chelsea pia ilitolewa kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 8-2 dhidi ya Paris Saint-Germain, kabla ya kufungwa 3-0 na Everton katika wiki hiyo hiyo.