Cole: Mbappe mchezaji bora duniani

Thursday February 18 2021
mbape pic

STAA wa zamani wa Ligi Kuu England, Joe Cole amemwaga sifa nyingi kwa Kylian Mbappe akisema ni mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa baada ya kupiga hat-trick kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Nou Camp mbele ya Lionel Messi aliyeitanguliza Barca kwa penalti.

Mbappe alifanya mambo yake hatari wakati alipoisaidia Paris Saint-Germain kuichapa Barcelona 4-1 juzi Jumanne uwanjani Nou Camp. Na Cole, 39, anaamini kwa sasa Mbappe yupo kwenye anga jingine kabisa dhidi ya Messi na Cristiano Ronaldo kwenye suala la mchezaji bora wa dunia.

“Mbappe ni mchezaji bora wa dunia. Umuhimu aliokuwa nao kwenye timu yake na namna anavyowakimbia wachezaji ni balaa.”

Advertisement