Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yasajili mabeki Pauni 360m

Muktasari:

  • Chelsea imefanikiwa kunasa saini ya Hato, ambaye alikuwa akiwindwa pia na miamba mingine ya Ligi Kuu England, Liverpool na Arsenal.

LONDON, ENGLAND: KUWASILI Kwa Jorrel Hato kwa ada ya Pauni 37 milioni kwenye kikosi cha Chelsea kimefanya miamba hiyo ya Stamford Bridge kuweka rekodi ya kutumia Pauni 360 milioni kusajili mabeki chini ya mmiliki mpya.

Chelsea imefanikiwa kunasa saini ya Hato, ambaye alikuwa akiwindwa pia na miamba mingine ya Ligi Kuu England, Liverpool na Arsenal.

Mdachi huyo sasa amekuwa beki wa 12 kusajiliwa na Chelsea tangu ilipoanza kuwa chini ya umiliki mpya, Clearlake Capital na bilionea Todd Boehly walipoinunua klabu hiyo, Mei 2022.

Lakini, Cucurella, ambaye alishinda ubingwa wa Euro 2024 akiwa na Hispania, anabaki kuwa beki pekee kwenye kikosi cha Chelsea kutajwa kuwa ni beki wa kiwango cha dunia. Na kama Chelsea inataka kushinda ubingwa wa ndani na ule wa Ulaya, inahitaji mabeki wengi zaidi wenye viwango vya juu.

Kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca kimeshabeba ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu, wakati ilipoichapa Paris Saint-Germain 3-0 katika fainali hizo zilizofanyika Marekani.

Chelsea imekusanya mabeki kibao akiwamo Levi Colwill, Trevoh Chalobah na Malo Gusto, ambao wamekuwa wakipambana kuifanya timu hiyo kufanya vizuri sambamba na Reece James.


MABEKI WOTE WALIONASWA CHELSEA CHINI YA TAJIRI BOEHLY

-Kalidou Koulibaly, Pauni 35milioni

-Marc Cucurella, Pauni 62milioni

-Wesley Fofana, Pauni 75milioni

-Benoit Badiashile, Pauni 35milioni

-Malo Gusto, Pauni 30.7milioni

-Axel Disasi, Pauni 38milioni

-Tosin Adarabioyo, bure

-Caleb Wiley, Pauni 8.5milioni

-Renato Veiga, Pauni 11.75milioni

-Aaron Anselmino, Pauni 15.6milioni

-Mamadou Sarr, Pauni 12milioni

-Jorrel Hato, Pauni 37milioni