Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yamfuta kazi Rosenior, McFarlane kuchukua mikoba

Muktasari:

  • Chelsea imeeleza kwamba haikuwa rahisi kufikia uamuzi huo lakini ililazimika kufanya hivyo kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo ambayo imekumbana na vipigo vitano mfululizo katika Ligi Kuu ya England bila kufunga bao, ikiwa ni rekodi yao mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 114.

LONDON, ENGLAND: KLABU ya Chelsea imetangaza rasmi kuachana na kocha Liam Rosenior, kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo ikiwa ni miezi mitatu na nusu tangu achukue mikoba ya Enzo Maresca.

Chelsea imeeleza kwamba haikuwa rahisi kufikia uamuzi huo lakini ililazimika kufanya hivyo kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo ambayo imekumbana na vipigo vitano mfululizo katika Ligi Kuu ya England bila kufunga bao, ikiwa ni rekodi yao mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 114.

Katika taarifa hiyo, klabu hiyo ilisisitiza kuwa matokeo mabovu pamoja na kiwango cha timu vimeshindwa kufikia viwango vinavyotarajiwa.

Hali hiyo imeongeza presha kwa uongozi kuchukua hatua hiyo mapema ili kujaribu kuokoa mpango wa kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao. Pamoja na uamuzi huo, Chelsea ilitoa shukrani kwa Rosenior na benchi lake la ufundi kwa mchango wao ndani ya kipindi walichokaa klabuni hapo.

Uongozi ulieleza kuwa Rosenior alionyesha uadilifu, nidhamu na weledi mkubwa tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo. Baada ya kuondoka kwake, Chelsea imemtangaza Calum McFarlane kuwa kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.

McFarlane atasaidiwa na benchi la ufundi lililopo huku jukumu lake likiwa kuiongoza timu katika kipindi hiki kigumu. 

Malengo makubwa kwa sasa ni kuhakikisha timu inafuzu michuano ya Ulaya na kufanya vizuri katika Kombe la FA.

Wakati huo huo, klabu imeanza mchakato wa kujitathmini ili kupata kocha wa muda mrefu atakayerejesha utulivu na mafanikio ndani ya timu.