Chelsea watajiwa bei ya Haaland

LONDON, ENGLAND. CHELSEA inahangaika na kusaka huduma ya Erling Haaland kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini Borussia Dortmund ilichowaambia kwamba staa huyo anauzwa Pauni 172 milioni.

Miamba mingine ya Ulaya inayosaka huduma ya mshambuliaji huyo ni Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Manchester United.

The Blues wenyewe wanaonekana kuwa mbelembele baada ya mmiliki wake bilionea Roman Abramovich kupata kutumia Pauni 154.5 milioni kwenye usajili wa mshambuliaji huyo na ishu itabaki kwa Dortmund kama watakubali kufanya biashara.

Kwa mujibu wa mwaandishi wa habari, Kristof Terreur, hatima ya Haaland haieleweki na kusema kuwapo na mazungumzo na mabingwa wa Ulaya, Chelsea.

Aliambia The Football Terrace: “Nafahamu kuna mazungumzo na mawakala wake, lakini Haaland ni mgumu sana kumtabiri. Ni ngumu hasa baada ya Dortmund kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, nina uhakika hiyo ni sababu ya kumbakiza. Lakini, Haaland ni mchezaji ambaye kila mtu anamtaka na anasubiriwa kwelikweli.”