Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harry Maguire bado hakijaeleweka Man United

Muktasari:

  • Klabu hiyo bado haijafikia mwafaka wowote katika mazungumzo yao ya kumsajili beki huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

MANCHESTER United bado inatafakari kuhusu hatma ya beki wao wa kimataifa wa England, Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 32.

Klabu hiyo bado haijafikia mwafaka wowote katika mazungumzo yao ya kumsajili beki huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya timu za Italia na Uturuki tayari zimewasiliana na wawakilishi Tnwake kuangalia uwezekano wa kumsajili.

Licha ya kuwindwa na timu mbalimbali, ripoti zinadai kipaumbele cha kwanza cha Maguire ni kuendelea kusalia Man United na ataondoka ikiwa mazungumzo ya mkataba mpya yatafeli.

Klabu kadhaa za Seria A ikiwemo Napoli zimeonyesha nia ya kumsajili staa huyu na tayari zimewasiliana na wawakilishi wake lakini hadi sasa hazijapewa majibu ya kueleweka.

Tangu kuanza kwa msimu huu Maguire amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

Man United inaripotiwa kuwa tayari kumsainisha Maguire mkataba mpya lakini inataka kwanza akubali kupunguza kiasi cha mshahara alichonacho kwa sasa.


Randal Kolo Muani

JUVENTUS imeongeza kasi katika harakati zao za kumsajili straika wa Ufaransa, Randal Kolo Muani, 27, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Tottenham Hotspur akitokea Paris Saint-Germain. Vigogo hao wa Italia wanaamini wanaweza kuweka ofa nono ambayo itamwezesha Muani  kuondoka. Ripoti nyingine zinadai Juventus inataka kuhamia kwa Muani baada ya kuona Tottenham imeanza mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta.


Joshua Zirkzee

STRAIKA wa kimataifa wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24, ameibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao Juventus inahitaji kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Manchester United inadaiwa kuwa tayari kumruhusu Zirkzee kuondoka kwa mkopo ikiwa itapatikana ofa itakayowavutia. Mkataba wa sasa wa Zirkzee unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote.


Kenan Yildiz

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Uturuki, Kenan Yildiz, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England England yupo  karibu kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Juventus. Nyota huyo alizivutia timu nyingi kutokana na kiwango boa alichoonyesha tangu msimu uliopita akiwa na Juventus. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Leon Goretzka

ATLETICO Madrid inatajwa kuwa na mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Leon Goretzka, mwenye umri wa miaka 30, ambaye mkataba wake wa sasa untarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. Inaelezwa Goretzka yuko kujiunga na timu hiyo ya La Liga akiamini itampa nafasi ya kupata changamoto mpya baada ya kutumika kwa muda mrefu katika Bundesliga.

Kocha Diego Simeone ameshazungumza na fundi huyu na kumhakikishia kwamba akijiunga nao atakuwa sehemu ya wachezaji wake tegemeo.


Jesse Lingard

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard, 33, yuko kwenye mazungumzo na klabu kadhaa za England na Italia. Lingard, ambaye ameshacheza mechi 32 za kimataifa, kwa sasa yupo huru baada ya kuondoka FC Seoul ya Korea Kusini, Desemba mwaka jana. Kwa sasa Lingard bado anafikiria ofa gani zaidi itamfaa kwani tayari baadhi ya klabu zimeshaonyesha nia ya kumsajili baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wake.


Kyle Walker-Peters

FIORENTINA, imetuma maombi kwenda West Ham United kuangalia uwezekano wa kumsajili beki wa timu hiyo na England, Kyle Walker-Peters, 28, na kiungo wa kati wa Ufaransa, Soungoutou Magassa, 22. Fiorentina inataka kuongeza nguvu katika safu yao ya ulinzi na kiungo kutokana na changamoto, sehemu ambazo zimekuwa na changamoto kwa msimu huu.


Radu Dragusin

AC Milan ipo sokoni kutafuta beki na sasa inataka kumsajili Radu Dragusin wa Tottenham, 23. Dragusin pia amekuwa akiwindwa na Roma na Napoli, hali inayofanya mchakato wa kumsajili kuwa mgumu kwa upande wa Milan. Milan inaamini staa huyu ataongeza nguvu katika safu yao ya ulinzi. Hadi sasa bado hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa, lakini mazungumzo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.