Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea kulazimika kumsajili Sancho

TETESI Pict

Muktasari:

  • wikiendi iliyopita ambao umewahakikishia kumaliza nafasi 15 za juu. Katika mkataba wa mkopo wa Sancho kulikuwa na kipengele ambacho kinawataka kumsainisha mazima ikiwa watamaliza nafasi 15 za juu katika msimamo.

CHELSEA watalazimika kulipa Pauni 5 milioni na kumrudisha Jadon Sancho katika timu yake ya Manchester United au kutoa karibu Pauni 25 milioni na kumsainisha mkataba wa kudumu.

Ulazima wa Chelsea kufanya hivyo unatokana na ushindi  wa wikiendi iliyopita ambao umewahakikishia kumaliza nafasi 15 za juu. Katika mkataba wa mkopo wa Sancho kulikuwa na kipengele ambacho kinawataka kumsainisha mazima ikiwa watamaliza nafasi 15 za juu katika msimamo.

Hata hivyo, ili kuepuka hilo wanaweza kulipa Pauni 5 milioni kama fidia kisha kumrudisha Man United. Mkataba wa sasa wa Sancho unatarajiwa kumalizika mwakani na msimu huu amecheza mechi 35 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti 10.


Rodri

MABOSI wa Real Madrid wanapambana kutaka kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri, 28, katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, lakini changamoto kubwa ni kwa Rodri mwenyewe ambaye hana mpango wa kuondoka kwa sasa. Staa huyo kwa sasa yupo nje kutokana na majeraha aliyopata tangu mwaka jana. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unamalizika 2027.


Moise Kean

MSHAMBULIAJI wa Fiorentina, Moise Kean ana kipengele katika mkataba wake ambacho kinamruhusu kuondoka kwa Pauni 45 milioni kati ya Julai 1 hadi 15 katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hata hivyo, licha ya kuhusishwa na timu mbalimbali  Ulaya anadaiwa kutaka kubaki Fiorentina akiamini itampa nafasi ya kuchaguliwa katika kikosi cha Italia kitakachokwenda kushiriki Kombe la Dunia 2026.


Michael Keane

EVERTON wapo tayari kumruhusu beki wa kati raia wa England, Michael Keane, 32, kuondoka klabuni mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. Kiwango cha beki huyo kinadaiwa kutomkosha kocha David Moyes ambaye ametoa ruhusu kwamba auzwe. Msimu huu Keane amecheza mechi 15 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Wojciech Szczesny

MKURUGENZI wa michezo wa Barcelona, Deco de Souza, ameweka wazi kwamba kipa wao raia wa Poland, Wojciech Szczesny, 35, atasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kubaki katika klabu hiyo. Staa huyo ambaye alisajiliwa na Barca Oktoba mwaka jana, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.


Xavi Simons

MSHAMBULIAJI wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons anaweza kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu, lakini ikiwa timu inayomtaka italipa kiasi kisichopungua Pauni 70 milioni. Kiasi hicho cha pesa kimewekwa rasmi kama bei na mabosi wa Leipzig kwa ajili ya kumuuza nyota huyo ambaye ni tegemeo katika kikosi chao cha kwanza.

Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa timu zinazomhitaji.


Diogo Jota

LIVERPOOL wanapanga kufanya mazungumzo kuamua hatma ya mshambuliaji raia wa Colombia, Luiz Diaz 28, msham-buliaji Mreno Diogo Jota (pichani), 28, na beki wa kati Mfaransa Ibrahima Konate, 25, wanapokaribia dirisha la usajili la kiangazi. Mastaa hao pia mikataba yao si mirefu, hivyo Liverpool inataka kuwaongeza kabla haijakaribia kwisha kabisa.


Georginio Rutter

CHELSEA wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Ufaransa, Georginio Rut-ter ambaye wanataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi mwaka huu. Rutter ameingia kwenye rada za Chelsea baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora akicheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao manane.