Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea kufungulia geti mastaa sita

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Kocha Enzo Maresca kwa sasa kina wachezaji kibao ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza. Kabla ya mechi za Jumamosi, Chelsea ilikuwa inashika nafasi ya nne katika msimamo, pointi 10 nyuma ya vinara Arsenal.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA itawafungulia mlango wa kutokea mastaa kibao wa Chelsea dirisha la Januari baada ya kuripotiwa wachezaji wasiopungua sita wataondoka Stamford Bridge.

Kikosi hicho cha Kocha Enzo Maresca kwa sasa kina wachezaji kibao ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza. Kabla ya mechi za Jumamosi, Chelsea ilikuwa inashika nafasi ya nne katika msimamo, pointi 10 nyuma ya vinara Arsenal.

Dirisha la usajili wa Januari ni fursa kubwa kwa klabu kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya kushindania ubingwa.

Hata hivyo, klabu ni lazima ziondoe wachezaji kwenye kikosi na  Chelsea itawaonyesha mlango wa kutokea wachezaji wasiopungua sita wataondoka Stamford Bridge kwa mujibu wa The Athletic.

Mchezaji mmoja wa Chelsea ambaye ataomba kuondoka ni mkali wa zamani wa Manchester City na Liverpool, Raheem Sterling. Winga huyo analipwa mshahara wa Pauni 325,000 kwa wiki na mkataba wake utaisha 2027 na hajacheza mechi yoyote.

CHEL 01

Chelsea bado haijapata timu ya kumnunua Sterling, lakini mchezaji huyo anataka kuondoka jumla baada ya kugomea uhamisho wa mkopo dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Axel Disasi ni mchezaji mwingine ambaye Maresca atahitaji aondoke kikosini. Wachezaji wengine ambao wanaripotiwa anaweza kufunguliwa mlango wa kutokea ni Filip Jorgensen, Deivid Washington, Sam Rak-Sakyi na Tyrique George.


MASTAA WALIOTOLEWA KWA MKOPO NA CHELSEA

Mike Penders (Strasbourg, Ufaransa)

Mamadou Sarr (Strasbourg, Ufaransa)

Kendry Paez (Strasbourg, Ufaransa)

Nicolas Jackson (Bayern Munich, Ujerumani)

Aaron Anselmino (Borussia Dortmund, Ujerumani)

David Datro Fofana (Fatih Karagumruk, Uturuki)