Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Arsenal atuma ujumbe mzito kwa wenzake

SALIBA Pict

Muktasari:

Arsenal ilisherehekea Krismasi kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na pia imetinga nusu fainali ya Kombe la Ligi na ipo kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako inaongoza msimamo wa jumla baada ya mechi sita.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa kati wa Arsenal, William Saliba amewaambia wachezaji wenzake: Sasa ni muda wa kubeba mataji.

Arsenal ilisherehekea Krismasi kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na pia imetinga nusu fainali ya Kombe la Ligi na ipo kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako inaongoza msimamo wa jumla baada ya mechi sita.

“Tunafahamu kwamba kila michuano tunayoshiriki tuna uwezo wa kushinda ubingwa,” amesema Saliba.

“Tulikaribia kubeba taji la Ligi Kuu England kwa misimu mitatu iliyopita na msimu uliopita tulifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi, hivyo tunafahamu tunapaswa kushinda kila taji.

"Lakini, tunapaswa kulionyesha hilo uwanjani na tunapaswa kuanzia sasa kushinda mataji. Ari ni nzuri na hii ndio kwanza Desemba, na tunafahamu vitu vinatokea kwa haraka sana kwenye soka, tunapaswa kutuliza akili yetu.”

Beki huyo Mfaransa aliongeza: “Bila shaka tunataka kushinda ubingwa wa kila mashindano, na tunafahamu tupo kwenye nusu fainali, hivyo kuna mechi tatu mbele yetu na tuna shughuli pevu Januari dhidi ya Chelsea.

“Hiyo itakuwa mechi ngumu, mechi kubwa, lazima tupambane. Tunafahamu tulikaribia kushinda ubingwa huo nyuma, hivyo tumejifunza mengi, hasa msimu uliopita. Tunataka kushinda ubingwa wa kila mashindano tunayocheza.”

Arsenal itacheza mechi tatu ndani ya wiki kutoka sasa hadi katikati ya Februari, lakini Saliba amesema: “Ndiyo, kama tuna mechi nyingi, hiyo ina maana tunahitaji kufanya kazi nzuri na bila ya shaka, wachezaji wetu majeruhi watarudi Januari kutusaidia kwa sababu tupo kwenye kila mashindano na tunataka kufanya vizuri.”