Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea ikimpata Simons kazi mnayo

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kwa pamoja, Simons na Palmer watafanya safu ya ushambuliaji ya Chelsea kuwa moto na tishio kubwa msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: STAA wa RB Leipzig, Xavi Simons anaweza kuwa mtu sahihi kwenda kumpunguzia mzigo wa kutengeneza nafasi za mabao mchezaji Cole Palmer huko Chelsea.

Kwa pamoja, Simons na Palmer watafanya safu ya ushambuliaji ya Chelsea kuwa moto na tishio kubwa msimu ujao.

Palmer, 23, ni mchezeshaji wa Chelsea, akihusika kwenye mambo muhimu kuifanya timu hiyo kuwa matata ndani ya uwanja.

Kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, Palmer alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Paris Saint-Germain.

Lakini, pindi staa huyo wa Three Lions anapokuwa kwenye kiwango cha chini kama ilivyokuwa nusu ya pili ya msimu uliopita, Chelsea ilikuwa kwenye hali mbaya katika ishu ya kutengeneza nafasi za mabao na kufunga.

Kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca kinahitaji staa mwingine mbunifu na mtengenezaji mwenye uwezo wa kupenya ngome ya ulinzi ya timu pinzani ili kuja kwenye kikosi chao kumsaidia Palmer.

Miamba hiyo ya Stamford Bridge imekuwa ikihusishwa pia na mpango wa kumchukua staa wa Aston Villa, Morgan Rogers, mkali wa Crystal Palace, Eberechi Eze na Alejandro Garnacho wa Manchester United.

Lakini, takwimu zinaonyesha kwamba Simons, anayethaminishwa kuwa na thamani ya Pauni 60 milioni, ndiye mwenye akili na viwango vinavyolingana na vya Palmer. Na hapo kama kocha Maresca atafanikiwa kuwa na huduma ya mastaa hao wawili Palmer na Simons kwa pamoja, basi beki za timu pinzani kwenye Ligi Kuu England msimu ujao, zitakuwa kwenye wakati mgumu.

Simons ni aina ya Palmer anayetumia mguu wa kulia, ambaye amekuwa akipenda kucheza akitokea upande wa kushoto wakati staa wa England, anapenda kucheza kutokea upande wa kulia, huku akiwa anatumia mguu wa kushoto. Na wote wamekuwa na kiwango bora cha ubunifu ndani ya uwanja tofauti na kile ambacho Rogers, Eze na Garnacho wamekuwa wakifanya.

Simons alikuwa na kiwango kizuri kwenye Bundesliga msimu uliopita, ambapo alifunga mabao 10 na kuasisti saba katika mechi 25, wakati Palmer alifunga mabao 15 na kuasisti manane katika mechi 37 kwenye Ligi Kuu England.