Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea buana!Eti wao sio Arsenal

Muktasari:

  • Mamia ya mashabiki wa tim hiyo walikuwa nje ya uwanja huo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton, usiku wa jana Jumanne, ambapo The Blues iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Chelsea wametoa mpya baada ya kubeba mabango yaliyoandikwa “Sisi sio Arsenal” wakati walipoandamana nje ya Uwanja wa Stamford Bridge kupinga umiliki wa bilionea Todd Boehly.

Mamia ya mashabiki wa tim hiyo walikuwa nje ya uwanja huo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton, usiku wa jana Jumanne, ambapo The Blues iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mara ya kwanza, mashabiki hao walipita Fulham Road wakiwa na mabango na kusababisha foleni kubwa barabarani, kabla ya kurusha miale ya moto na kuangusha chini noti za dola.

Kituo cha usafiri wa treni huko Fulham Broadway kilifungwa kwa muda kutokana na miale hiyo ya moto, huku ikiripotiwa kwamba zimamoto walilazimika kuitwa kwenda kuweka hali sawa hasa kwa kile kilichokuwa kikitokea nje ya Uwanja wa Stamford Bridge.

Mashabiki wa Chelsea wamecharuka baada ya timu yao kupoteza mechi tatu mfululizo katika michuano yote. Kabla ya mchezo huo wa usiku wa Jumanne, Chelsea ilikuwa imeshinda mechi tatu tu kati ya 12 zilizopita.

Mashabiki hao walichukizwa na namna mambo yanavyokwenda na wengine walisikika wakiimba nyimbo za Roman Abramovich nje ya Stamford Bridge.

Bilionea wa Kimarekani, Boehly, aliinunua Chelsea 2022 na tangu wakati huo amewekeza Pauni 1.2 bilioni kwenye usajili, huku Chelsea ikipita chini makocha wakuu watatu tofauti na wengine kadhaa wa muda.

Ushindi wao wa juzi dhidi ya Southampton umewaingiza kwenye Top Four ya Ligi Kuu England kabla ya mechi za Jumatano, huku mashabiki wengi wasiwasi wao nbi kama timu itashindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.