Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CD Colunga kumtumia kipa wa miaka 70 Ligi daraja la tano Hispania

UMRI Pict (1)

Muktasari:

  • Mhispania huyo ambaye alistaafu soka la ushindani miaka 27 iliyopita anatarajiwa kucheza kama kipa wa timu ya Asturias CD Colunga katika mchezo wa Ligi ya Daraja la Tano Jumapili hii. Iwapo atacheza kama ilivyopangwa na kuvaa glovu atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kushiriki katika mechi rasmi nchini Uhispania.

MADRID, HISPANIA: KATIKA umri ambapo wachezaji wengi wa zamani wa soka wangependelea kukaa wakiwasimulia wajukuu, marafiki na watu wa karibu baa hadithi tamu kuhusu umahiri wao wa zamani uwanjani, Angel Mateos Gonzalez mwenye umri wa miaka 70 anarejea tena uwanjani.

Mhispania huyo ambaye alistaafu soka la ushindani miaka 27 iliyopita anatarajiwa kucheza kama kipa wa timu ya Asturias CD Colunga katika mchezo wa Ligi ya Daraja la Tano Jumapili hii. Iwapo atacheza kama ilivyopangwa na kuvaa glovu atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kushiriki katika mechi rasmi nchini Uhispania.

Mateos, ambaye amekuwa akiwasaidia makipa wa Colunga katika msimu huu wa mashindano ya Tercera Federacion kundi la pili, amesema bado hajui kama atacheza kwa dakika zote 90. “Ninafanya mazoezi na timu, lakini bado sijui kama nitacheza mechi nzima au nusu ya kwanza tu,” amesema katika mahojiano na gazeti la eneo hilo El Comercio.

UMR 01

Katika chapisho la Facebook, timu hiyo ya Kaskazini mwa Hispania ilisema imeamua kumtumia Mateos katika mchezo dhidi ya wapinzani wa eneo hilo, CD Praviano, kama njia ya kumheshimu kipa huyo na kujitolea kwake maisha yote katika kazi na soka.

Klabu hiyo ilisema hatua hiyo siyo ya maonyesho uwanjani kwamba watakuwa na mkongwe, bali ni kutambua mtu anayewakilisha maadili yao.

“Mateos anawakilisha kikamilifu tunachosimamia hapa CD Colunga yaani mapenzi, uthabiti, heshima katika soka na namna ya kuchukulia mchezo ambayo inapita umri,” ilisema taarifa hiyo.

“Umri siyo jambo muhimu. Kilicho muhimu ni mtazamo, kujitolea na uaminifu kwa mchezo. Tunazungumzia mtu ambaye alikuwa mchimba migodi ambaye amejitolea maisha yake kwenye kazi na soka, na ambaye amekuwa akiwasaidia makipa wetu msimu mzima.”

UMR 02

Klabu hiyo iliongeza kuwa, “Mateos hachezi kwa sababu ana miaka 70. Anacheza kwa sababu ameistahili.”

Mchezaji huyo wa zamani wa migodi aliiambia El Comercio kwamba ingawa amekuwa akijitunza akiwa na afya bora na kwamba soka limebadilika kidogo tofauti na zamani. “Nilipoanza, ilikuwa ni mchezo tofauti kabisa. Mipira; viwanja … nakumbuka nilikuwa na ndoo kando ya lango ili kumwaga maji wakati uwanja unajaa matope, jambo ambalo lilikuwa karibu kila siku wakati huo,” amesema.

Mateos aliiambia redio ya Cope kwamba amekuwa akicheza soka tangu akiwa na miaka 10 na bado ana uzito uleule wa kilo 68 au 69, na kama alivyokuwa akiwa na miaka 18 pia ni mtu mwenye ushindani mkali na kwamba hapendi kushindwa kwenye aina yoyote ya mchezo.