Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick apigiwa debe Man United

CARIC Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno yuko kwenye shinikizo kubwa Old Trafford baada ya kuanza vibaya msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United wameshaambiwa wafanye uamuzi wenye busara na kumchukua Michael Carrick ikiwa itaachana na Ruben Amorim.

Kocha huyo Mreno yuko kwenye shinikizo kubwa Old Trafford baada ya kuanza vibaya msimu huu.

Mashetani hao wekundu walitolewa katika Kombe la Carabao na Grimsby Town na sasa wako nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Man United pia ina tofauti ya pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja na pointi nabe nyuma ya viongozi wa ligi, Liverpool, baada ya michezo minne.

Huu ndiyo mwanzo mbaya zaidi wa msimu wa Ligi Kuu England tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya mwaka 1992.

Wadau wengi wanaona Amorim yuko karibu kuondoka katika timu hiyo kutokana na matokeo ambayo amekuwa akiyapata.

Kocha wa zamani msaidizi wa Man United, Rene Meulensteen, 61, anaamini Carrick angekuwa mbadala bora wa kuirudisha klabu kwenye nafasi nzuri katika ligi ikiwa Amorim ataondoka.

"Michael Carrick anaweza kuwa chaguo sahihi ikiwa Ruben Amorim ataondoka. Ni wazi, Carrick bado anafahamu wachezaji wengi waliokuwapo alipokuwa pale. Hivyo bado ana taarifa nzuri za ndani. Anafahamu klabu vizuri. Anajua kinachotarajiwa kutoka kwa klabu. Jose Mourinho pia yupo nje ya kazi ingawa kuna makocha wengine pia. Lakini muhimu ni kuwa na mtu ambaye ana uzoefu na timu, pia atakayeweka mfumo ambao wachezaji wanauunga mkono. Kwa sababu waliopo sio wachezaji wabaya, kuna wachezaji wengi wazuri pale."

Carrick, 44, yupo huru baada ya kutokuwa na klabu tangu alipoachishwa kazi Middlesbrough Juni mwaka huu.

Hata hivyo, si huru kabisa kwani amekubali kufanya uchambuzi katika kituo cha Prime Video katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Carrick alitumia miaka 12 ya kazi yake ya uchezaji kama mchezaji wa kawaida Old Trafford chini ya Sir Alex Ferguson.

Wakati huo, alishinda mataji matano ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kuteuliwa kuwa nahodha wa klabu mwaka 2017.

Pia aliwahi kuongoza mechi tatu kama kocha wa muda wa Man United baada ya Ole Gunnar Solskjaer kuachishwa kazi mwaka 2021.

Alishinda mbili kati ya mechi zake tatu akiwa kocha akiongoza ushindi dhidi ya Villarreal na Arsenal kabla ya sare na Chelsea.