Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick apewa mikoba Manchester United

CARRICK Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu atachukua mikoba kutoka kwa aliyekuwa mchezaji mwenzake na kiungo mwenzake wa zamani, Darren Fletcher, katika benchi la ufundi la Old Trafford, ambaye alikuwa kocha wa kipindi cha mpito, akiinoa timu hiyo kwenye mechi mbili.

MANCHESTER, ENGLAND: MICHAEL Carrick amekubali kuwa kocha wa muda wa Manchester United hadi mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu atachukua mikoba kutoka kwa aliyekuwa mchezaji mwenzake na kiungo mwenzake wa zamani, Darren Fletcher, katika benchi la ufundi la Old Trafford, ambaye alikuwa kocha wa kipindi cha mpito, akiinoa timu hiyo kwenye mechi mbili.

Fletcher alipandishwa kutoka nafasi yake ya kocha wa kikosi cha U-18 ili kuiongoza timu dhidi ya Burnley na Brighton baada ya  kufukuzwa kwa Ruben Amorim, Jumatatu iliyopita.

Alisimamia sare ya 2-2 katika Uwanja wa Turf Moor, kabla ya Man United kutolewa kwenye Kombe la FA baada ya aliyekuwa mshambuliaji wao Danny Welbeck kufunga bao la ushindi kwa Brighton katika mechi iliyofanyika Old Trafford na kuchapwa 2-1.

CARR 01

Sasa Carrick atakuwa kocha mkuu wa muda hadi majira ya kiangazi. Carrick, mshindi wa Ligi Kuu England mara tano, 44, aliwahi kuiongoza Man United katika mechi tatu kama kocha wa mpito mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya Ole Gunnar Solskjaer kufukuzwa, kabla ya Ralf Rangnick kuja kama kocha wa muda.

Cha kushangaza, Carrick ndiye aliyemshinda Solskjaer katika kuwania nafasi hii ya sasa baada ya Man United kuzungumza na wote wawili. Baada ya kipindi chake kifupi Old Trafford, Carrick alikaa kwa miaka mitatu kama kocha wa Middlesbrough, akishinda karibu nusu ya mechi zake 136 alizoongoza.

CARR 02

Middlesbrough ilimaliza nafasi ya nne, nane na kumi chini ya Carrick katika Championship, lakini alifukuzwa kazi mwishoni mwa msimu uliopita.

Carrick atasimamia mechi 17, akianza na dabi ya Manchester uwanjani Old Trafford, Jumamosi hii, huku Man United ikiwa tayari wametolewa kwenye Kombe la FA  na Kombe la Ligi na pia walishindwa kufuzu kushiriki michuano ya Ulaya.

Hii inamaanisha Man United itacheza jumla ya mechi 40 tu msimu huu, mechi 38 za Ligi Kuu, moja FA Cup dhidi ya Brighton, na kipigo cha kushtua katika Kombe la Ligi dhidi ya Grimsby, idadi ambayo ni ndogo zaidi tangu msimu wa 1914–1915.

Carrick anaungwa mkono na Cristiano Ronaldo katika jukumu lake la muda. Mwanasoka huyo maarufu wa Ureno alitumia mtandao wa X kuonyesha hadharani kumuunga mkono aliyekuwa mchezaji mwenzake. Ronaldo alishea picha yao wakiwa pamoja baada ya mechi ya kwanza ya Carrick kama kocha mwaka 2021 na mchango wake uliisaidia Man United kushinda ugenini dhidi ya Villarreal.

CARR 03

Mshindi wa Ballon d’Or mara tano amesema: “Michael Carrick alikuwa mchezaji wa kiwango cha juu sana, na anaweza pia kuwa kocha bora. Hakuna lisilowezekana kwa mtu huyu. Binafsi, ninajivunia kucheza naye bega kwa bega, na pia kufanya kazi naye akiwa kocha wetu benchini.”

Staa mwingine wa Man United, Wayne Rooney naye amejitolea yupo tayari kwenda kuwa msaidizi wa Carrick.

Rooney amesema: “Klabu imepoteza utambulisho wake, imepoteza ile hali ya kifamilia, kama unavyoweza kusema. Hii ni fursa ya kuirejesha hali hiyo, kuirudisha roho ya Manchester United ndani ya klabu.”