Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Roque avunja ukimya dili la kurudi Ulaya

ROQUE Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Palmeiras ya Brazil amekiri kwamba anauona mustakabali wake ukimrejesha Ulaya.

NYOTA anayewaniwa na klabu za Man Utd na Chelsea, Vitor Roque amethibitisha mipango yake ya kutaka kurudi Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa Palmeiras ya Brazil amekiri kwamba anauona mustakabali wake ukimrejesha Ulaya.

Fowadi huyo kinda, baada ya kipindi kisichofanikiwa huko Barcelona, ameweza kujijenga upya Palmeiras mwaka huu.

Roque sasa amezivutia klabu za Manchester United na Chelsea, huku wakala wake Andre Cury akisema uhamisho kwenda Ligi Kuu ya England huenda ukatokea mwaka 2026.

“Nilienda Ulaya nikiwa bado mdogo sana. Nilijifunza mengi kutokana na uzoefu huo. Vile vile, kurejea soka la Brazil si hatua ya kurudi nyuma, kinyume chake kabisa," ameliambia Aliliambia gazeti AS na kuongeza;

“Wakati mwingine unahitaji kurudi hatua moja ili kupiga hatua mbili mbele. Luiz Henrique pia ni uthibitisho wa hilo; alirudi na kutwaa mataji akiwa na Botafogo. Natumai kufuata njia hiyo hiyo: kurudi na kushinda mataji.”

Zaidi ya hayo, Roque mwenyewe alisisitiza dhamira yake, akisema:

“Ni ndoto pia kurejea Ulaya na kuzoea. Mwenyezi Mungu akipenda, nitaendelea kufanya kazi yangu Palmeiras, kwa sababu hilo ndilo lengo langu kwa sasa, na siku za usoni nitarudi Ulaya.”