Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher ataka watatu Liverpool

Muktasari:

  • Carragher alieleza kuwa matumizi makubwa ya fedha yaliyofanywa na Liverpool msimu uliopita hayakuzaa matunda yaliyotarajiwa ambapo klabu hiyo ilitumia kiasi cha pauni 446 milioni kusajili nyota wapya, ikiwa ni rekodi mpya katika historia ya ligi hiyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: NYOTA wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher ametoa wito kwa klabu hiyo kubadili mkakati wake wa usajili na kurejea katika mfumo uliowaletea mafanikio hapo awali, kufuatia kipigo cha mabao 3-2 walichopata dhidi ya mahasimu wao Manchester United mwishoni mwa wiki.

Carragher alieleza kuwa matumizi makubwa ya fedha yaliyofanywa na Liverpool msimu uliopita hayakuzaa matunda yaliyotarajiwa ambapo klabu hiyo ilitumia kiasi cha pauni 446 milioni kusajili nyota wapya, ikiwa ni rekodi mpya katika historia ya ligi hiyo.

Miongoni mwa usajili ghali uliofanywa ni Hugo Ekitike, Florian Wirtz na Alexander Isak, ambao walikuwa miongoni mwa wachezaji waliogharimu fedha nyingi zaidi.

Hata hivyo, pamoja na matarajio makubwa, Liverpool imeshindwa kuendana na ushindani na kwa sasa ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 58 baada ya mechi 35, ikiwa nyuma kwa pointi 18 dhidi ya vinara Arsenal.

“Watu wengi walifurahia matumizi ya fedha yaliyofanywa kiangazi kilichopita lakini haikuwa tabia ya Liverpool tuliyoizoea chini ya Jurgen Klopp. Ilionekana kama klabu inayonunua nyota kwa bei kubwa bila mpango maalum,” alisema.

Kwa mujibu wa Carragher, Liverpool inapaswa kuimarisha maeneo matatu muhimu, winga wa kulia, beki wa kulia na kiungo wa kati.

Pia aligusia kuwa kuondoka kwa wachezaji muhimu kama Mohamed Salah na Andrew Robertson mwishoni mwa msimu kutaacha pengo kubwa ambalo linahitaji kuzibwa haraka.

Aliongeza kuwa klabu hiyo haihitaji kufanya usajili wa wachezaji wengi kwa wakati mmoja, bali wachague wachache watakaoingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuongeza ubora.

Kwa sasa, Liverpool imepoteza michezo 11 msimu huu, jambo linaloonyesha wazi kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kurejea katika ubora uliowahi kuifanya kuwa moja ya timu bora barani Ulaya.