Cameroon yaisikilizia Brazil

DOHA, QATAR. CAMEROON imeambulia sare ya mabao 3-3 dhidi ya Serbia huku kipa wao chaguo namba moja kwenye kikosi Andre Onana akitimuliwa kambini kutokana na utovu wa nidhamu.
Cameroon ilihitaji ushindi kujiweka salama kabla ya mchezo wao mwisho dhidi ya Brazil hatua ya makundi.
Mashabiki wa Cameroon waliofurika uwanja wa Al Janoub walivurugwa baada ya Cameroon kuwa nyuma kwa maabo 3-1 na kupoteza matumaini yao ya kusonga mbele raundi inayofuata.
Hata hivyo Cameroon ilisawazisha mabao mawili dakika ua 63 na 66 kupitia Vincent Aboubakar na Eric Maxim Choup-Moting, bao lao la kuongoza liliwekwa kimiani na Jean-Charles Castelletto dakika ya 29.
Mabao ya Serbia yalifungwa na Strahinja Pavlović dakika ya 45, Sergej Milinković-Savić dakika ya 45 zikiwa zimebaki dakika tatu za nyongeza mpira kuelekea mapumziko, na Aleksandar Mitrović aliyepachika msumari wao mwisho dakika 53.
Sasa Cameroon ina kibarua kizito dhidi ya Brazil kwenye mechi yao ya mwisho hatua ya makundi.