Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Caicedo ni pengo kubwa Chelsea

Muktasari:

  • Kiungo wa Ecuador, Caicedo, 24, amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea msimu huu, hivyo kukosekana kwake uwanjani kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu kutaleta madhara makubwa kwa timu hiyo ya Stamford Bridge.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA iliweza kupambana jino kwa jino na vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal baada ya kumpoteza kiungo Moises Caicedo, lakini ilikuja kuonyesha kiwango cha hovyo dhidi ya timu inayopambana isishuke daraja.

Kiungo wa Ecuador, Caicedo, 24, amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea msimu huu, hivyo kukosekana kwake uwanjani kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu kutaleta madhara makubwa kwa timu hiyo ya Stamford Bridge.

Chelsea baada ya kushuhudia kukosa huduma ya Cole Palmer kutokana na maumivu, mambo hayakuonekana kuwa magumu kwao kutokana na uwepo wa Caicedo, ambaye sasa amekuwa shida kutokana na kukosekana.

Jambo hilo lilionekana kwenye mechi ya Jumatano usiku, ambapo Chelsea ilichapwa na Leeds United. Katika mechi hiyo, Chelsea ilipoteza vita zote na ilifanya makosa makubwa ambayo Caicedo mara nyingi amekuwa akiyafanyia kazi.

Tangu aliponaswa kwa Pauni 115 milioni kutoka Brighton, Caicedo amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho na kuwaondoa The Blues kwenye presha ya kumkosa Palmer.

Chelsea imeshinda robo tu ya mechi zake za Ligi Kuu England ilizocheza bila ya huduma ya Caicedo, wakati iliibuka na ushindi kwa asilimia 52 ya mechi ilizocheza wakati kiungo huyo wa shoka alipokuwa uwanjani.

Kiungo mwenzake pacha, Enzo Fernandez, amekuwa hana maajabu makubwa pindi anapocheza bila ya uwepo wa Caicedo na katika mchezo wa Leeds United alifanya makosa mengi na kumpa kazi Andrey Santos, ambaye alishindwa kuvaa vyema buti za Caicedo. Kocha Enzo Maresca alisema: “Tumemkosa Moi na tutakwenda kumkosa Moi mechi ijayo.”

Chelsea ilikabiliwa na mechi ya Bournemouth jana Jumamosi huku Caicedo atakosa pia mechi dhidi ya Everton, Des 13. Jambo hilo linaifanya Chelsea kucheza mechi nyingi bila yake.