Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yaipunguzia Morocco adhabu matukio fainali za AFCON 2025

Muktasari:

  • Senegal iliifunga Morocco bao 1-0 kwenye fainali iliyochezwa Januari 18, 2026, katika mechi iliyogubikwa na sintofahamu baada ya wachezaji wa Senegal kugoma kuendelea kucheza kufuatia waandaaji kupewa penalti dakika za majeruhi huku matokeo yakiwa bado 0-0.

MOROCCO imetangazwa kuwa bingwa wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kubatilisha matokeo ya kipigo chao kwenye fainali dhidi ya Senegal kufuatia tukio la utata la kutoka uwanjani.

Senegal iliifunga Morocco bao 1-0 kwenye fainali iliyochezwa Januari 18, 2026, katika mechi iliyogubikwa na sintofahamu baada ya wachezaji wa Senegal kugoma kuendelea kucheza kufuatia waandaaji kupewa penalti dakika za majeruhi huku matokeo yakiwa bado 0-0.

Baada ya kusimama kwa takriban dakika 17, wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani ambapo penalti ya Brahim Diaz iliokolewa, kabla ya Pape Gueye wa Senegal kufunga bao la ushindi katika muda wa nyongeza.

Hata hivyo, matokeo hayo sasa yamebatilishwa na chombo kinachosimamia soka barani Afrika.

Katika taarifa yake, CAF imesema Senegal imechukuliwa kuwa imepoteza mechi ya fainali kwa kujitoa na kwamba matokeo ya mechi yameandikwa kuwa ushindi wa mabao 3-0 kwa Morocco.

Uamuzi huo umefuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF), ambayo CAF imesema imekubalika kisheria na imeamuliwa kwa faida yao.

Caf imeongeza kuwa, Senegal ilikiuka Kifungu cha 82 cha kanuni za AFCON, jambo lililosababisha kutumika kwa Kifungu cha 84.

Kifungu cha 82 kinaeleza kuwa ikiwa timu itakataa kucheza au itaondoka uwanjani kabla ya muda wa kawaida kuisha bila ruhusa ya mwamuzi, itachukuliwa kama imepoteza na itaondolewa kwenye mashindano.

Kifungu cha 84 kinaongeza kuwa timu yoyote itakayokiuka Kifungu cha 82 itaondolewa kabisa kwenye mashindano na kupoteza mechi hiyo kwa mabao 3-0.

Bodi ya Rufaa ya CAF haikuishia tu kuivua Senegal ubingwa, pia ilibatilisha na kupunguza baadhi ya adhabu zilizokuwa zimetolewa awali kwa Morocco na Bodi ya Nidhamu ya CAF:


Maamuzi mengine muhimu:

1. Adhabu ya kufungiwa hadi Mechi 3 kwa Saibari kwa kuingilia taulo la golikipa wa Senegal imepunguzwa hadi mechi 2, na faini yake ya dola 100,000 imefutwa kabisa.

2. Faini ya dola 200,000 iliyotozwa Morocco kwa tabia ya watoto wa kuokota mipira (ball boys) kwenye fainali imepunguzwa hadi dola 50,000.

3. Faini ya dola 15,000 iliyotozwa Morocco kwa mashabiki wao kutumia laser wakati wa fainali pia imepunguzwa hadi dola 10,000.

4. Faini ya Laser Lights imepungua kutoka dola 15000 hadi dola10000

Bodi ya Rufaa ya CAF iliyoamua Senegal wapokwe ubingwa:

PRESIDENT: Jaji Roli Daibo Harriman

VICE: Faustino Monteiro


MEMBERS

Moez Ben Tahar

Musa Ikanqa

Hamoud Bowbe

Mohamed Djama

Asogbavi Komlan

Jaji Masauko

Lubamba Hector