Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Evra aishangaa CAF, asema imeshusha heshima ya soka la Afrika

Muktasari:

  • Evra amedai kuwa kitendo hicho ni 'kujishusha thamani' kwa soka la bara hilo na kusema dunia nzima sasa inaitizama Afrika kwa kicheko.

Gwiji wa soka wa Ufaransa mwenye asili ya Senegal, Patrice Evra, amemwaga povu zito kufuatia uamuzi wa CAF wa kuivua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuipatia Morocco.

Evra amedai kuwa kitendo hicho ni 'kujishusha thamani' kwa soka la bara hilo na kusema dunia nzima sasa inaitizama Afrika kwa kicheko.

"Nilivyoiona taarifa ya Morocco kuwa mabingwa, nilijua ni siku ya wajinga (April Fool’s)," amesema Evra huku akisisitiza kuwa bingwa wa kweli uwanjani ni Senegal. 🇸


Nini kimetokea?

Uamuzi huu unakuja baada ya CAF kubatilisha matokeo ya fainali ya Januari 18, 2026, ambapo Senegal iliondoka uwanjani kulalamikia penalti ya dakika za lala salama.

ESPN na vyanzo vingine vimeripoti kuwa Morocco sasa wametangazwa washindi wa 3-0 kwa kanuni za Forfeit (Kushindwa kufika au kukataa kuendelea na mchezo).

Shirikisho la Soka ya Senegal (FSF) tayari limetangaza kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Unakubaliana na Evra? Je, ubingwa huu wa Morocco ni wa halali au Senegal wameonewa?