Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BROWN: Mwamba wa NBA anayepiga kote kote

ATM Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, ni wachezaji wachache ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuingiza kipato cha kutosha kupitia biashara huku bado wakiendelea kucheza.

BOSTON, MAREKANI: Katika ulimwengu wa michezo, hasa mpira wa kikapu, wachezaji wengi wamekuwa wakipata mikataba minono inayowaingizia pesa na kuwafanya kuishi maisha ya kifahari.

Hata hivyo, ni wachezaji wachache ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuingiza kipato cha kutosha kupitia biashara huku bado wakiendelea kucheza.

Jaylen Brown, nyota wa Boston Celtics inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya NBA, ni miongoni mwa wachezaji hao. Hapa tunakusogezea utajiri wake kamili na namna anavyopiga pesa ndani na nje ya uwanja.

AT 05

ANAPIGAJE PESA

Julai 2023, Jaylen Brown aliweka historia kwa kusaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya dola 304 milioni (zaidi ya shilingi 790 bilioni za Kitanzania) na Boston Celtics. Huu ni mkataba mkubwa zaidi katika historia ya NBA, unaompatia wastani wa zaidi ya dola 60 milioni kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Forbes, Brown anaingiza mapato ya jumla yanayokaribia dola 80 milioni mwaka 2025, ikiwa ni pamoja na bonasi na madili yake ya nje ya uwanja.

Staa huyu alikataa kuwa balozi wa kampuni yoyote ya viatu na badala yake alianzisha kampuni yake binafsi ya viatu inayoitwa Seven Forty-One.

Mwaka 2024, alizindua kiatu chake cha kwanza chenye lebo yake yake, The Rover, na kilipokewa vizuri na mashabiki.

Mbali na kuwa na kampuni hiyo, Brown ana mikataba ya udhamini na kampuni kadhaa kama Beats by Dre, Pepsi, na Oakley. Kwa ujumla, anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia dola 80 milioni.

AT 01

MSAADA KWA JAMII

Brown amekuwa na msaada mkubwa kwa jamii kwani ni mwanzilishi wa shirika liitwalo Boston XChange aliloanzisha ili kukuza ustawi wa kifedha na ubunifu katika jamii zisizo na huduma za kifedha.

Pia amekuwa balozi wa kampeni ya Boston Creator Incubator + Accelerator yenye lengo la kusaidia wajasiriamali kwa kuwapa mtaji na mwongozo.

Alihusika pia katika kampeni ya 675 inayolenga kusaidia watu wenye ulemavu kupitia mpira wa kikapu.

AT 03

NDINGA

Porsche Macan – Dola 80,000

Range Rover Sport – Dola 60,000

Mercedes-Benz G-Wagon – Dola 90,000

AT 02

NYUMBA

Ana nyumba mbili. Ya kwanza ni ile ya Seaport, Boston yenye vyumba vitatu vyenye choo ndani yake, pia ina maeneo mengine kama sehemu ya kutazama filamu, eneo la kupata vinywaji na sehemu ya kufanyia mazoezi yake binafsi.

Mjengo huo una thamani ya dola 4.75 milioni.

Nyumba nyingine ya kifahari anayomiliki ni ile ya Wellesley, Massachusetts, yenye vyumba saba, mabafu nane, ukumbi wa sinema na uwanja wa michezo. Hii inakadiriwa kuwa na thamani ya dola 10.2 milioni.

AT 04

BATA NA MAISHA BINAFSI

Staa huyu yupo katika uhusiano na mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu, Kysre Gondrezick.

Julai 2024, walionekana wote kwa mara ya kwanza walipokuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya Kysre ambapo walikwenda Brazil. Pia mwaka huo walionekana kwenye hafla ya tamasha la 2024 ESPYs.

Brown pia anapenda sana kujifunza na kwa sasa anadaiwa kuweza kuzungumza lugha nyingine mbili mbali na Kiingereza ambazo ni Kihispania na Kiarabu.