Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Bayern Munich ahofia Kane kuondoka

BOSI Pict

Muktasari:

  • Rais wa heshima wa klabu hiyo, Uli Hoeness, ameweka wazi kuwa wanataka kumbakiza Kane licha ya tetesi za klabu zenye nguvu kifedha.

MUNICH, UJERUMANI: UONGOZI wa Bayern Munich ya Ujerumani umeanza kuwa na hofu juu ya mshambuliaji wao hatari, Harry Kane kuwa anaweza kushawishika kuondoka kutokana na ofa kubwa ambazo zinaweza kumimika kutoka Saudi Arabia.

Rais wa heshima wa klabu hiyo, Uli Hoeness, ameweka wazi kuwa wanataka kumbakiza Kane licha ya tetesi za klabu zenye nguvu kifedha.

Bayern kwa sasa wanafanya juhudi za kuongeza mkataba wa Kane ambao unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, huku wakitaka kuhakikisha anaendelea kubaki Allianz Arena kwa muda mrefu zaidi.

Ripoti zinaonyesha kuwa mkataba mpya unaweza kuongeza mshahara wake hadi kufikia pauni 400,000 kwa wiki, jambo litakalomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi duniani.

Hali hii inakuja baada ya Kane kutotumia kipengele cha kuondoka (release clause) kilichokuwa kimewekwa kwenye mkataba wake na kilichoisha mapema mwaka huu. Hata hivyo, Hoeness anakiri wazi kuwa nguvu ya fedha kutoka Saudi Arabia inaweza kumshawishi mchezaji yeyote, licha ya kuwa na furaha Ujerumani.

Mpaka sasa Kane amefunga mabao 31 na kutoa pasi 5 za mabao katika mechi 26 za Bundesliga pamoja na mabao 10 katika mechi 9 za Ligi ya Mabingwa.

Kutokana na kiwango hicho, Hoeness ameweka wazi kuwa thamani ya Kane inaweza kufikia hadi euro 250 milioni, akisisitiza kuwa ni ada kubwa sana inayoweza kuwazuia wanaomtaka.