Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Blatter arudi Fifa, Bin Hammam apinga kuondolewa

Sepp Blatter,Rais Fifa

ZURICH, Uswisi Katika hatua nyingine, mgombea wa nafasi hiyo ya urais wa Fifa, Mohamed Bin Hammam ameandika barua Fifa kulalamika kuwa hakutendewa haki na kuondolewa jina lake katika kinyang'anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo. Bin Hammam alisema kuwa madai ya rushwa anayodaiwa, yalilenga kumharibia mpango wake wa kuingia Fifa. Kiongozi huyo wa Shirikisho la Soka Asia, AFC anadaiwa kuhonga wajumbe wa Ukanda wa Concacaf ili wampe kura katika uchaguzi wa jana. Bosi huyo wa Qatari aliamua kuondoa jina lake. "Licha ya [Bin Hammam's] kuondoa jina, hakukata rufani na alikataa kuingia kwenye mkutano wa Fifa," ilisema tovuti ya Bin Hammam. "Hakukuwa na uhalali wa mimi kusimamishwa. Hakukuwa na umuhimu wa kunisimamisha eti waanze uchunguzi, lakini hapa ni wazi wameanzisha misigano na kusababisha maumivu yasiyo na msingi." Taarifa ilisema kuwa hatua ya kumsimamisha Bin Hammam haikutokana na Kamati ya maadili. "Kusimamishwa kwangu ni maamuzi ya mwenyekiti na si kamati ya maadili. Hatua ya mwenyekiti si dharura, kupandikiza kutoelewana. "Kutokana na hili lisilokuwa la haki, Mohamed Bin Hammam amejiweka pembeni, anapinga uamuzi uliotolewa kuwa si wa haki wala kutofuata sheria na kanuni."