Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bingwa Wimbledon afungiwa miaka minne

BINGWA Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo kutoka Jamhuri ya Czech alidai alikataa kumruhusu afisa wa vipimo kuingia nyumbani kwake kwa sababu alihofia usalama wake kutokana na msongo mkubwa wa mawazo aliokuwa nao kipindi hicho.

LONDON, ENGLAND: BINGWA wa Wimbledon wa mwaka 2023, Marketa Vondrousova, amefungiwa miaka minne kujihusisha na mchezo wa tenisi baada ya kukataa kufanyiwa kipimo cha dawa za kuongeza nguvu.

Mchezaji huyo kutoka Jamhuri ya Czech alidai alikataa kumruhusu afisa wa vipimo kuingia nyumbani kwake kwa sababu alihofia usalama wake kutokana na msongo mkubwa wa mawazo aliokuwa nao kipindi hicho.

Hata hivyo, Mahakama huru pamoja na Shirika la Kimataifa la Uadilifu wa Tenisi (ITIA) zimeeleza kuwa kukataa kipimo ni kosa kubwa linalofanana na kukutwa na dawa hizo mwilini.

ITIA imesisitiza kuwa adhabu kali ni muhimu ili kuzuia wachezaji kukwepa vipimo kwa makusudi.

BING 01

Kwa adhabu hiyo, Vondrousova mwenye umri wa miaka 26 atarejea uwanjani akiwa na miaka 30, hali inayoweza kuweka hatarini mustakabali wa maisha yake ya tenisi.

Adhabu ya kufungiwa kwa miaka minne inaweza kuonekana kuwa kali sana, hasa ikilinganishwa na mchezaji Jenson Brooksby, ambaye alifungiwa miezi 18, adhabu ambayo baadaye ilipunguzwa hadi miezi 13, baada ya kukosa vipimo vitatu vya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Sababu ya tofauti hiyo ni kwamba kukataa kabisa kupimwa kunachukuliwa kuwa kosa kubwa zaidi kuliko kukosa kipimo.

Mamlaka zinaamini kuwa adhabu lazima iwe kali ili kuzuia wachezaji wanaotumia dawa hizo kukwepa vipimo kwa makusudi wakitegemea kupata adhabu ndogo.

BING 02

Mtendaji Mkuu wa International Tennis Integrity Agency (ITIA), Karen Moorhouse, amesema kuwa usalama na ustawi wa wachezaji pamoja na maafisa wa vipimo ni jambo la msingi.

Alieleza kuwa maafisa hao wamepewa mafunzo ya kitaalamu, na shahidi anayeshuhudia zoezi la upimaji huwa wa jinsia moja na mchezaji anayepimwa.

Pia hubeba vitambulisho rasmi muda wote, na wachezaji wana nafasi ya kuthibitisha utambulisho wao kwa njia nyingine endapo watakuwa na mashaka.

Moorhouse aliongeza kuwa vipimo vya kushtukiza ni sehemu muhimu ya kulinda uadilifu wa mchezo wa tenisi, na kwamba jopo huru lililotoa uamuzi lilikubaliana na msimamo huo.

BING 03

Alisisitiza kuwa kesi hii ni ukumbusho kwa wachezaji wote kwamba wanaweza kupimwa wakati wowote na mahali popote, na kwamba kukataa kupimwa kunaweza kusababisha adhabu kubwa.

ITIA pia ilithibitisha kuwa Vondrousova aliwasilisha ushahidi wa kitabibu unaoonyesha kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la afya ya akili. Hata hivyo, taasisi hiyo ilisema haiwezi kutoa maoni kuhusu uamuzi wa jopo huru, ambao utachapishwa baadaye, na kusisitiza kuwa kiwango cha kukubali utetezi wa aina hiyo ni cha juu sana.

Vondrousova ana umri wa miaka 26 kwa sasa, hivyo atakuwa na miaka 30 wakati adhabu yake itakapomalizika. Kwa kuzingatia ugumu wa kurejea kwenye kiwango chake bora baada ya kukaa nje ya mchezo kwa miaka minne, adhabu hiyo inaweza kuwa karibu kumaliza kabisa maisha yake ya soka la tenisi.