Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biliadi ya Bibi kuipa England bahati ya ubingwa?

Muktasari:

  • Bibi huyo, Lynne Brown mwenye umri wa miaka 68 kutoka Overland Park, Kansas, amefichua kuwa aliwauzia viongozi wa timu ya England meza ya kuchezea biliadi (pool), mchezo maarufu unaochezwa kwa kugongesha mipira kwenye meza maalumu kwa kutumia fimbo ndefu na kuingiza mipira hiyo kwenye matundu yaliyopo pembezoni mwa meza.

KANSAS CITY, MAREKANI: WAKATI timu ya England ikiendelea na harakati za kusaka taji la Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani, kuna kisa kutoka Kansas City kimeibuka na kuwa gumzo baada ya bibi mmoja kudai anaweza kuwa sehemu ya siri ya mafanikio ya kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel.

Bibi huyo, Lynne Brown mwenye umri wa miaka 68 kutoka Overland Park, Kansas, amefichua kuwa aliwauzia viongozi wa timu ya England meza ya kuchezea biliadi (pool), mchezo maarufu unaochezwa kwa kugongesha mipira kwenye meza maalumu kwa kutumia fimbo ndefu na kuingiza mipira hiyo kwenye matundu yaliyopo pembezoni mwa meza.

Brown alisema awali aliitangaza meza hiyo kwenye Facebook Marketplace kwa lengo la kuuza baada ya familia yake kupanga kufanya ukarabati wa sehemu ya chini ya nyumba yao, lakini hakutarajia wanunuzi wangekuwa kutoka kambini kwa England.

Kwa mujibu wa Brown, alipokea ujumbe kutoka kwa watu waliodai kuwa wanawakilisha timu inayoshiriki Kombe la Dunia iliyoweka kambi Kansas City, kabla ya kubaini baadaye kuwa walikuwa watu wa England.

"Kwa mwanzo sikujua ni timu gani. Nilikuwa nahisi labda ni England lakini sikuwa na uhakika," alisema Brown akizungumza na vyombo vya habari vya Marekani.

Haikuchukua muda mrefu kwa makubaliano kufikiwa kwani jioni hiyo kundi kubwa la wafanyakazi wa England liliwasili nyumbani kwake likiwa na lori kubwa kwa ajili ya kubeba meza hiyo.

Brown alisema iliwachukua watu watano hadi sita wenye miili mikubwa kuiondoa meza hiyo kutokana na uzito wake mkubwa huku wakilazimika kusimama njiani mara kadhaa kabla ya kuipakia.

Meza hiyo ilinunuliwa kwa dola 700 za Marekani, zaidi ya Sh1.8 milioni za Kitanzania huku mume wa Brown akitaka kufanya mazungumzo ya kupata tiketi za Kombe la Dunia badala ya fedha.

"Mume wangu alisema tuombe tiketi, lakini nilimwambia meza hii haiwezi kuwa na thamani sawa na tiketi za Kombe la Dunia," alisema Brown huku akicheka.

Licha ya kukosa tiketi hizo, Brown sasa anaamini meza hiyo inaweza kuwa sehemu ya siri ya kujenga mshikamano na burudani kwa nyota wa England kambini wakati wakijiandaa na mechi zao za Kombe la Dunia.

Kwa utani, bibi huyo amesema iwapo England itafanikiwa kutwaa Kombe la Dunia mwezi ujao, basi yeye atachukua sehemu ya sifa za ushindi huo.