Benzema, Kante watwaa ubingwa Saudia
Muktasari:
- Al-Hilal waliokuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu uliopita wa kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na mchezo mmoja mkononi na kiujumla ikiwa imebakisha michezo mitatu ya ligi.
Al Ittihad ya Saudi Arabia imetangazwa kuwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya kufikisha pointi 77.
Ittihad ambayo huu ni ubingwa wao wa 10 ilifikisha pointi hizo baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Raed.
Al-Hilal waliokuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu uliopita wa kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na mchezo mmoja mkononi na kiujumla ikiwa imebakisha michezo mitatu ya ligi.
Kwa upande wa Ittihad hadi sasa imebakisha mechi mbili tu kutimiza idadi ya mechi 34 za ligi hiyo.
Wababe hawa kutoka Mji wa Jeddah wamechukua ubingwa kimahesabu, kwani timu pekee inayoweza kufikia pointi zao ni Al Hilal ikiwa itashinda mechi zote tatu na hata ikiifikia bado Ittihad itakuwa juu kutokana na kanuni za ligi.
Kanuni zinaeleza kwamba ikiwa timu zitafungana pointi, kitakachoangaliwa ni ipi imepata pointi nyingi zaidi pale zilipokutana.
Hata hivyo, timu hizi zote kila mmoja alimfunga mwenzake msimu huu na kwa sababu hiyo kanuni inaeleza kwamba kitakachoangaliwa baada ya hapo ni utofauti wa mabao pale zilipokutana.
Ittihadi ndio imefunga idadi kubwa zaidi ya mabao kujumla katika mechi zote mbili ilizokutana na Al-Hilal, hivyo ubingwa ni wao.