Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bega la Odegaard lashtua Arsenal

ODEGAD Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mchezeshaji alionekana kupatwa na maumivu ya bega kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Nottingham Forest, Jumamosi iliyopita.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta anakuna kichwa kutokana na kiungo na nahodha wake, Martin Odegaard kuwa na rekodi za kuumiaumia kwa siku za karibuni.

Kiungo huyo mchezeshaji alionekana kupatwa na maumivu ya bega kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Nottingham Forest, Jumamosi iliyopita.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Odegaard, 26, kuanza kwenye kikosi cha Arsenal tangu Agosti 23, wakati alipoumia bega kwa mara ya kwanza kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Leeds United. Kiungo huyo alicheza kwa dakika 20 tu kwenye mechi iliyofuatia dhidi ya Liverpool, wakati kikosi chake cha Arsenal kilipochapwa 1-0.

Odegaard alienda kucheza kwa dakika 45 wakati Norway ilipopata ushindi wa 1-0 dhidi ya Finland kwenye mechi ya kirafiki, kabla ya kucheza kwa dakika tisini dhidi ya Moldova. Staa huyo aling'ara wakati Norway ilipowasambaratisha wapinzani wao 11-1, huku mwenyewe akifunga bao moja na kuasisti mawili.

Jambo hilo lilimsukuma Arteta kumwanzisha Odegaard dhidi ya Forest, Jumamosi. Lakini, staa huyo wa zamani wa Real Madrid alikomea kwenye dakika ya 18 tu ya mchezo baada ya kutonesha bega lake na hivyo kuifanya Arsenal kuwa kwenye mashaka makubwa ya kumtumia kwenye mechi nguvu dhidi ya Athletic Bilbao na Manchester City.

Baada ya kupatiwa tiba, Odegaard alicheza kwa dakika 10 baadaye na kushindwa kuendelea, akatolewa na nafasi yake aliingizwa Ethan Nwaneri.

Katika mechi hiyo ya Forest, mabao ya Arsenal yalifungwa na Martin Zubimendi, aliyepachika nyavuni mara mbili na straika, Viktor Gyokeres alifunga mara moja.