Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern Munich yaiachia majanga Arsenal

TROS 01
TROS 01

Muktasari:

  • Trossard, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora zaidi msimu huu, alitolewa nje dakika ya 38 baada ya kushindwa kuendelea na mechi.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imepata pigo jingine katika safu yao ya ushambuliaji baada ya staa wao Leandro Trossard kulazimika kuondolewa uwanjani kutokana na jeraha wakati wa mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Trossard, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora zaidi msimu huu, alitolewa nje dakika ya 38 baada ya kushindwa kuendelea na mechi.

Mbelgiji huyo alitembea kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ili kupatiwa matibabu zaidi na nafasi yake ikachukuliwa na Noni Madueke.

Trossard amehusika katika mabao 10 akiwa na Arsenal kwenye mechi 15 msimu huu, akifunga mabao matano na kutoa asisti  tano.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amelazimika kumtegemea Trossard kutokana na msururu wa majeraha kwa washambuliaji wa timu hiyo.

TROSSARD Pict

Madueke, aliyempokea Trossard, alikuwa amerudi uwanjani hivi karibuni baada ya jeraha la goti lililomweka nje tangu mwishoni mwa Septemba.

Mbali ya Madueke, Gabriel Martinelli naye alirekea kikosini Jumapili, huku kapteni Martin Odegaard, akirejea katika mechi dhidi ya Bayern.

Hadi sasa Arsenal bado inaelea kuwakosa Viktor Gyokeres, Kai Havertz na Gabriel Jesus katika safu ya ushambuliaji.