Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsene Wenger aitabiria ubingwa Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Arsenal kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi ya EPL baada ya mechi nane, ikiwa na pointi tatu zaidi ya Manchester City na nne mbele ya mabingwa watetezi Liverpool.

Aliyekuwa Kocha wa Arsenal, Arsène Wenger, amesema msimu huu 2025-2026 anaona tofauti kubwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kinachoongozwa na kocha Mikel Arteta, na huenda mambo yakawanyookea kwa kutwaa ubingwa.

Arsenal kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi ya EPL baada ya mechi nane, ikiwa na pointi tatu zaidi ya Manchester City na nne mbele ya mabingwa watetezi Liverpool.

The Gunners pia ni moja ya timu tatu pekee zilizoshinda mechi zao zote katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, baada ya kuibamiza Athletic Club, Olympiacos, na Atlético Madrid bila kuruhusu bao lolote.

Wenger, alipozungumza na beIN SPORTS kabla ya ushindi wa Arsenal wa 4-0 dhidi ya Atlético, aliulizwa kama The Gunners ni washindani halisi wa ubingwa msimun huu, alijibu: “Ndiyo, bila kusita hata kidogo.

“Unaweza kusema kwamba mimi husema hivyo kila mwaka, lakini naamini mwaka huu wako tayari kweli kukabiliana na changamoto zozote.

ARS 01

“Msimu uliopita walipowapoteza Kai Havertz na Bukayo Saka, ilikuwa pigo kubwa sana, lakini mwaka huu wana [Noni] Madueke… [Eberechi] Eze anaweza kumchukua nafasi [Martin] Ødegaard, wana [Gabriel] Martinelli, [Leandro] Trossard.

“Kwenye safu ya ulinzi wana [Cristhian] Mosquera, na pembeni pia wana wachezaji wa akiba. [Myles] Lewis-Skelly kwa sasa haingii hata kwenye kikosi cha kwanza, na bado yupo kwenye timu ya taifa ya England. Wana kikosi kamili zaidi.”

Wenger liiongoza Arsenal kwa miaka 22, akianza kazi mwaka 1996 na kuondoka klabuni hapo mwaka 2018.

Akiwa Arsenal, Wenger alifanikiwa kutwaa ubingwa wa EPL mara tatu  (1997–98, 2001–02, 2003–04), Kombe la FA mara saba (1998, 2002, 2003, 2005, 2014, 2015, 2017) na Ngao ya Jamii mara saba.