Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern kufanya pati ya ubingwa Jumapili

Muktasari:

  • Timu hiyo chini ya kocha Vincent Kompany itapanda kwenye eneo la wazi juu ya jengo la 'town hall' kusherehekea taji hilo la 34.

MUNICH, UJERUMANI: MIAMBA ya soka la Ujerumani,  Bayern Munich wataungana na mashabiki wao katika sherehe kubwa ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga 2025/26 itakayofanyika Marienplatz, Jumapili, Mei 17, 2026

Timu hiyo chini ya kocha Vincent Kompany itapanda kwenye eneo la wazi juu ya jengo la 'town hall' kusherehekea taji hilo la 34.

Siku inayofuata, Mei 18, meya mpya wa Munich, Dominik Krause, atapokea pia kikosi cha wanawake cha Bayern mjini humo ambapo watasaini kitabu cha wageni katika ukumbi mkuu wa Baraza na kupiga picha za kumbukumbu kwenye kwenye eneo la wazi juu ya jengo hilo.

Kwa sababu mechi ya mwisho ya wanawake wa Bayern itachezwa kesho, Jumapili dhidi ya Hamburg, sherehe ya pamoja ya timu zote mbili haitafanyika kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

Mashabiki ambao hawataweza kuhudhuria watafuatilia sherehe hizo kwa njia ya mtandao 'live stream' ya bure kwenye tovuti rasmi ya klabu hiyo pamoja na mitandao yao ya Facebook na YouTube, ikiwa na matangazo kwa lugha ya Kijerumani, Kiingereza na Kihispania.

Pia kutakuwa na blogu ya moja kwa moja itakayotoa picha na video kuonesha hali ya sherehe hizo kwa mashabiki duniani kote.