Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barua ya wazazi yamduwaza Saka

SAKA Pict

Muktasari:

  • Saka, 24, alisaini mkataba mpya wiki iliyopita ambao utaendelea kumbakiza katika kikosi hicho cha Emirates hadi 2030.

LONDON, ENGLAND: WINGA mwenye mshahara mkubwa kuzidi wote Arsenal, Bukayo Saka ameachwa mdomo wazi baada ya kupokea barua ya hisia kali kutoka kwa wazazi wake kutokana na kusaini mkataba wake mpya kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Saka, 24, alisaini mkataba mpya wiki iliyopita ambao utaendelea kumbakiza katika kikosi hicho cha Emirates hadi 2030.

Nyota huyo wa England alikabidhiwa barua hiyo kutoka kwa wazazi wake, Adenike na Yomi na akakosa maneno ya kuelezea hisia zake.

Wazazi wa Saka walieleza jinsi mioyo yao ilivyojaa fahari na wanajivunia jinsi mtoto wao alipofikia kwa sasa.

Adenike na Yomi waliandika: “Mkataba huu mpya ni uthibitisho, si tu wa kipaji chako, bali pia wa nidhamu yako, unyenyekevu na uimara wa tabia yako. Tunajivunia jinsi ambavyo umekuwa. Katika kila mafanikio na kila changamoto, umeendelea kubaki mnyenyekevu, mwema na mwenye shukrani.”

Saka alikabidhiwa barua hiyo na shirika la utangazaji la Marekani, CNN, lililomhoji baada ya kutangazwa kwa mkataba huo. Winga huyo alishikwa na hisia aliposoma maneno ya wazazi wake, ambao walihamia London kutoka Nigeria kabla yeye hajazaliwa.

Saka amesema: “Wow. Si mara nyingi namwona mama na baba wakizungumza nami kwa namna hii. Kwa kweli nimekosa maneno. Ni jambo la kushangaza. Sina la kusema zaidi ya kuwashukuru. Nisingekuwa hapa bila wao. Safari yao, kwangu, ni ya kutia moyo. Kutoka kuwa Nigeria hadi hapa tulipo leo kama familia, maelezo pekee ni Mungu. Si jambo la kawaida. Nafasi ni kama moja katika milioni. Nina shukrani sana na hili ni jambo zuri sana.”