Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yazidi kujisogeza kwa Marc Guehi, Liverpool nayo ipo

Muktasari:

  • Staa huyo mwenye umri wa miaka 25, mara kadhaa pia amekuwa akihusushws na Liverpool inayodaiwa kuwa bado haijakata tamaa katika mpango wa kumsajili. Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi Guehi alikuwa karibu kujiunga na Liverpool kwa ada iliyodaiwa kuwa Pauni 35 milioni, lakini mchakato ulikufa baada ya kocha wa Palace kuuzuia. Liverpool inamwangalia staa huyo kama mbadala sahihi wa Virgil van Dijk ambaye umri unazidi kumtupa mkono.

BARCELONA imejiingiza katika vita dhidi ya vigogo wengine Ulaya ili kuipata saini ya beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi ambaye imekuwa ikimfuatilia kwa karibu.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 25, mara kadhaa pia amekuwa akihusushws na Liverpool inayodaiwa kuwa bado haijakata tamaa katika mpango wa kumsajili. Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi Guehi alikuwa karibu kujiunga na Liverpool kwa ada iliyodaiwa kuwa Pauni 35 milioni, lakini mchakato ulikufa baada ya kocha wa Palace kuuzuia. Liverpool inamwangalia staa huyo kama mbadala sahihi wa Virgil van Dijk ambaye umri unazidi kumtupa mkono.

Kwa upande wa Barca imekuwa ikipambana kuweka sawa safu ya ulinzi kwa sababu imekuwa ikiruhusu mabao na Guehi anaonekana kuwa ataongeza chachu eneo hilo. Vilevile Barca imevutiwa sana na mchezaji huyo.


Gonzalo Garcia

BRIGHTON inamfuatiia kwa karibu  mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Garcia mwenye umri wa miaka 21, na inapanga kuwasilisha ofa ili kumsajili kwa mkopo wa nusu msimu ifikapo Januari, mwakani. Mbali ya Brighton fundi huyo pia anawindwa na klabu nyingine kama Leeds United na Sunderland. Garcia ni mmoja wa washambuliaji bora ndani ya kikosi cha Real Madrid na mara kadhaa amekuwa akionekana benchi katika kikosi cha wakubwa.


Kevin Filling

MANCHESTER United ipo vitani na Borussia Dortmund pamoja na timu nyingine Ulaya katika kuiwania saini ya mshambuluaji kinda kutoka Sweden, Kevin Filling, 19, kutoka AIK Fotboll Filling ambaye amekuwa akitazamwa na maskauti wa timu nyingi ambao wote wameonyesha kuvutiwa na kiwango chake. Mchezaji huyo amekuwa aikifananishwa sana na Alexander Isak wa Liverpool kutokana na aina ya uchezaji wake pamoja na umbo alilonalo.


Niclas Fullkrug

AC Milan imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa raia wa Ujerumani, Niclas Fullkrug, 32, ambaye tayari ameambiwa anaweza kuondoka West Ham United, Januari mwakani. Fullkrug amekuwa akipambana kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha West Ham, lakini mambo yanaonekana kuwa magumu. Awali ilidaiwa kuna uwezekano akatimkia timu za Ujerumani.


Antoine Semenyo

LIVERPOOL inaonekana mstari wa mbele kwenye harakati za kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25, kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi licha ya timu yake kutotaka kumuuza. Mbali ya Liverpool, Tottenham ipo kwenye mazungumzo na wawakilishi wake. Semenyo amekuwa akiwindwa na Liverpool kwa muda ikimwona kama mbadala wa Mohamed Salah.

Joshua Zirkzee

WEST Ham United, Everton na Roma zote zinamuwinda mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee, 24, na zinataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Zirkzee anayeweza kucheza kama namba tisa akishambulia na kusaidia kukaba, aliomba kuondoka Man United tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sababu hajioni katika mipango ya kocha wa sasa wa Mashetani Wekundu.


Nicolas Jackson

STRAIKA wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, 24, ambaye anacheza kwa mkopo Bayern Munich ataendelea kusalia katika timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu. Jackson aliripotiwa kuwa huenda akarejea Chelsea dirisha lijalo la majira ya baridi lakini mpango huo umekufa kwa sababu amekataa kwani anajisikia furaha kuendelea kusalia Ujerumani.


Joao Gomes

KIUNGO wa Wolves, Joao Gomes anadaiwa kuwaambia mabosi kwamba anataka kujiunga na Manchester United katika dirisha lijalo la majira ya baridi, baada ya timu hiyo kuonyesha nia ya kumsajili na kuwa tayari kulipa Pauni 44 milioni za ada ya uhamisho. Staa huyo Mbrazili, 24, amevutiwa na mipango ya kocha Ruben Amorim anayezungumza naye mara kwa mara.