Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca, Madrid zarudi mzigoni La Liga

LA LIGA Pict

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Real Madrid ilipigwa kikumbo kwenye ubingwa wa LaLiga na mahasimu wao Barcelona, huku kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, nako ilitupwa nje kwa aibu na Arsenal.

MADRID, HISPANIA: MCHAKAMCHAKA wa La Liga unaanza wikiendi hii, lakini kitu cha kushangaza kwa mara ya kwanza, Real Madrid itasubiri hadi Jumanne kucheza mechi yake ya kwanza kwenye michuano hiyo ya msimu huu.

Hizi zitakuwa zama mpya katika kikosi cha Los Blancos na sasa kitakuwa chini ya Xabi Alonso baada ya kuachana na Carlo Ancelotti.

Msimu uliopita, Real Madrid ilipigwa kikumbo kwenye ubingwa wa LaLiga na mahasimu wao Barcelona, huku kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, nako ilitupwa nje kwa aibu na Arsenal.

Licha ya kumsajili Kylian Mbappe, bado Madrid ilikuwa na mwaka mmoja, ulioendelea hadi kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu.

Lakini, wakati msimu mpya wa La Liga ukianza, Madrid inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa, huku mechi yake ya kwanza itakuwa Jumanne itakapokipiga na Osasuna. Hakuna sababu ya msingi ya mechi hiyo kupigwa Jumanne.

La Liga itaanza leo Ijumaa kwa mechi mbili na Girona itakipiga na Rayo Vallecano, wakati Villarreal itakuwa nyumbani kupepetana na Real Oviedo na baada ya hapo kutakuwa na mechi kila siku hadi Jumanne, Madrid itakapocheza.

Barcelona itacheza Jumamosi, ikianzia ugenini dhidi ya Real Mallorca, wakati Atletico Madrid itanza kibarua chake cha kusaka ubingwa wa La Liga, Jumapili kwa kumenyana na Espanyol.

Hivyo, Real Madrid itakuwa na faida ya kuona wapinzani wao wote jinsi walivyoanza msimu ili kujua ifanyeje katika mechi hiyo ya uwanjani Bernabeu.

Hata hivyo, kwenye mechi hiyo Madrid haitakuwa na huduma ya Jude Bellingham, ambaye atakuwa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega, huku Ferland Menday na Endrick nao wakiripotiwa ni majeruhi.

Eduardo Camavinga na Federico Valverde wanakimbizana na muda ili kucheza mechi hiyo kutokana na kuwa na majeraha ambayo yaliwafanya wakose mechi ya mwisho ya pre-season. Mikikimikiki ya La Liga msimu huu itashuhudia pia mechi ya Barcelona na Villarreal ikipigwa nje ya Hispania na itafanyika kwenye Uwanja wa Hard Rock, Miami, Marekani, Desemba 21.

Hata hivyo, Real Madrid inapinga mpango huo wa mechi ya La Liga kucheza nje ya Hispania.