Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balogun apambana kuvunja rekodi ya Mbappe Ligue 1

Muktasari:

  • Hata rekodi zake binafsi ziko hatarini. Mshambuliaji wa AS Monaco ya Ufaransa, Folarin Balogun ndiye mchezaji pekee aliyefunga katika mechi nane mfululizo msimu huu katika ligi kubwa Ulaya, rekodi ambayo anaweza kuivunja iwapo atafunga dhidi ya Toulouse, wikiendi hii.

PARIS, UFARANSA: HUU siyo msimu mzuri kwa pamoja kwa Kylian Mbappe. Real Madrid imepoteza Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa Ulaya na huenda hata LaLiga. Mbaya zaidi, Vedat Muriqi, straika wa mabao wa Real Mallorca anatishia nafasi yake kama mfungaji bora wa ligi akiwa na mabao 21 dhidi ya 23 ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid.

Hata rekodi zake binafsi ziko hatarini. Mshambuliaji wa AS Monaco ya Ufaransa, Folarin Balogun ndiye mchezaji pekee aliyefunga katika mechi nane mfululizo msimu huu katika ligi kubwa Ulaya, rekodi ambayo anaweza kuivunja iwapo atafunga dhidi ya Toulouse, wikiendi hii.

Mchezaji huyo wa zamani wa akademi ya Arsenal aliyesajiliwa kwa Euro 30 milioni mwaka 2023, tayari amewahi kutishia ubabe wa Mbappe wa tuzo ya Pichichi 2022–23. Tuzo hiyo hutolewa kila msimu kwa mchezaji anayefunga mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu Hispania (La Liga).

Wakati huo, Balogun alikuwa akiichezea Stade de Reims na alimaliza Ligue 1 akiwa na mabao 21, huku Mbappe akimaliza na 29.

Akiwa Monaco, hakuanza vizuri hasa kutokana na majeraha akifunga mabao manane 2023–24 na kumaliza 2024–25 akiwa nayo manne, lakini msimu huu hadi mwanzoni mwa Novemba alikuwa na matatu.

Lakini, ujio wa kocha Sebastien Pocognoli katikati ya Oktoba, mwaka jana akichukua nafasi ya Adi Hütter ulibadilisha mambo, ambapo mabao 17 kati ya 18 aliyofunga msimu huu (12 kwenye ligi) yamepatikana chini ya kocha huyo wa zamani wa Union Saint-Gilloise.

“Ameboresha uchezaji wake akiwa amegeukia lango, pasi zake zimeimarika na pia umaliziaji wake. Lakini, bado anataka kuendelea kujifunza na anapokea maelekezo," alisema Pocognoli.

Ni mchezaji mwenye ufanisi zaidi sasa na tunampa pasi nzuri. Tunatumia vyema uwezo wake mipira mirefu na nafasi wazi zinamfaa sana,” alisema mwenzake Jordan Teze.

“Najihisi huru zaidi na nina jukumu kubwa zaidi. Pocognoli ni kocha wa kipekee, anatupa mawazo mengi, ubunifu na uhuru, lakini pia ana nidhamu kali,” alisema Balogun, ambaye sasa analenga kuvunja rekodi ya mabao ya mfululizo katika Ligue 1 inayoshikiliwa na Mbrazili Sonny Anderson aliyefunga katika mechi 11 mfululizo akiwa na Olympique Lyon 2001.