Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bale: Sasa nacheza na watoto

Bale Pict
Bale Pict

Muktasari:

  • Staa huyo ambaye pia aliitumikia Tottenham aliamua kuachana na soka mwaka 2023 akiwa na umri wa miaka 33, baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Liverpool, England : STAA wa zamani wa Real Madrid, Gareth Bale amesema kwa sasa anafurahia sana maisha ya kustaafu soka kwa kuwa anapata muda mwingi wa kucheza gofu na kukaa na wanaye.

Staa huyo ambaye pia aliitumikia Tottenham aliamua kuachana na soka mwaka 2023 akiwa na umri wa miaka 33, baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Bale, wakati anacheza soka alitwaa makombe matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa mmoja kati ya wachezaji waliofanikiwa zaidi kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya. Juzi alikuwa mmoja kati ya wachambuzi kwenye kituo cha TNT wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid.

“Nina furaha sana kurejea tena kwenye soka, nimekuwa nikitumia muda mwingi kwenye gofu, kuliko kuhangaika na soka.

“Nimekuwa napata muda mwingi sana kucheza na watoto wangu, ukiwa unacheza soka kila siku unakuwa umechoka na kulala kwenye vyumba tofauti, lakini sasa nafurahi sana kuwa karibu na familia yangu,” alisema Bale ambaye kwenye maisha yake ya soka alicheza mechi 553 na kufunga mabao 185.