Balaa la Bundesliga, La Liga usipime!
Muktasari:
- Kwenye La Liga zitapiga mechi nne leo Jumamosi na Leganes itamaliza ubishi na Alaves, wakati Osasuna itaikaribisha Real Madrid, Real Madrid na Celta Vigo huku Villarreal itakuwa na kasheshe kwa Valencia.
MADRID, HISPANIA: UTAMU kolea. Ndicho unachoweza kusema kuhusu vipute vya wikiendi hii kwenye La Liga na Bundesliga.
Kwenye La Liga zitapiga mechi nne leo Jumamosi na Leganes itamaliza ubishi na Alaves, wakati Osasuna itaikaribisha Real Madrid, Real Madrid na Celta Vigo huku Villarreal itakuwa na kasheshe kwa Valencia.
Kesho, Jumapili, zitapigwa nje nyingine, Espanyol na Athletic Bilbao, Real Valladolid na Sevilla, Mallorca na Las Palmas, wakati Real Betis itapepetana na Real Sociedad.
Bundesliga nako ni moto juu ya moto na Bayer Leverkusen itakipiga na Bayern Munich, VfL Bochum na Borussia Dortmund, huku Union Berlin ikicheza na Borusia Monchegladback, VfB Stuttgart na Wolfsburg na St Pauli itacheza na Freiburg, kabla ya kesho kushuhudia vipute vya Werder Bremen itakayokuwa nyumbani kucheza na Hoffenheim, wakati Eintracht Frankfurt itakipiga na Holstein Kiel na FC Heidenheim na Mainz 05.