Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bafana Bafana yamtia mashaka kocha Broos

BAFANA Pict

Muktasari:

  • Katika ushindi wao wa kwanza wa mabao 2-1 dhidi ya Angola huko Marrakesh, Bafana Bafana ilipunguza kasi baada ya kupata bao la kuongoza na kuruhusu Palancas Negras kusawazisha. Afrika Kusini walifunga mapema lakini walishindwa kwenda mapumziko ikiwa mbele.

CASABLANCA, MOROCCO: KOCHA wa Bafana Bafana, Hugo Broos, ana wasiwasi kuhusu kushindwa kwa timu yake kukosa ukatili wa kumaliza mechi katika nyakati muhimu wakati ikishiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 huko Morocco.

Broos amesema Afrika Kusini imekuwa na udhaifu wa kushindwa kumaliza mechi pindi inapofanikiwa kumbana vilivyo mpinzani.

Katika ushindi wao wa kwanza wa mabao 2-1 dhidi ya Angola huko Marrakesh, Bafana Bafana ilipunguza kasi baada ya kupata bao la kuongoza na kuruhusu Palancas Negras kusawazisha. Afrika Kusini walifunga mapema lakini walishindwa kwenda mapumziko ikiwa mbele.

Kulikuwa na vipindi vingi katika mechi dhidi ya Angola ambavyo Afrika Kusini haikuvishughulikia vizuri. Hali hiyo pia ilijitokeza katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Misri iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani huko Agadir Ijumaa, pamoja na ushindi mgumu wa 3-2 dhidi ya Zimbabwe huko Marrakesh Jumatatu uliowawezesha Bafana kufuzu hatua ya 16 bora.

Broos hakufurahishwa na jinsi Bafana walivyowaacha Zimbabwe warudi kwenye mchezo mara mbili, huku katika baadhi ya vipindi Warriors wakitawala mchezo.

Bafana watakutana na Ivory Coast au Cameroon mjini Rabat katika raundi ya 16 bora ya mtoano Jumapili, na Broos aliweka wazi hawatakuwa na nafasi yoyote ikiwa wataendelea kuwa laini na kukosa ukatili wa kumaliza mechi.

“Hili ni jambo linalonitia wasiwasi kwa sababu limetokea tena katika mchezo huu na dhidi ya Zimbabwe. Hata katika kipindi cha kwanza dhidi ya Misri, tulikuwa laini na dhaifu, hatukuwa na dhamira katika mapambano na hakukuwa na ukatili,”  amesema Broos.

“Tulianza kwa uchokozi katika dakika 20 za mwanzo dhidi ya Zimbabwe, lakini tukapunguza kasi na kuwapa wapinzani nafasi ya kurudi kwenye mchezo. Lazima tujifunze kuwa na umakini kwa sababu raundi inayofuata ni Ivory Coast au Cameroon, na hatuwezi kucheza kwa namna hiyo dhidi yao. Tukifanya hivyo, hatutakuwa na nafasi ya kushinda mchezo huo.”