Bacary Sagna afunguka uchungu wa kufiwa
Muktasari:
- Staa huyo wa Ufaransa alijaribu kwa kupambana sana kusahau maumivu yaliyomkabili wakati alipofiwa na kaka yake. Omar, ambaye alifariki dunia siku moja kabla ya kutimiza umri wa miaka 28, Februari 2008.
LIVERPOOL, ENGLAND: BACARY Sagna amefunguka ya moyoni akidai anafahamu maumivu wanayopata wanasoka wanapopoteza wapendwa wao.
Staa huyo wa Ufaransa alijaribu kwa kupambana sana kusahau maumivu yaliyomkabili wakati alipofiwa na kaka yake. Omar, ambaye alifariki dunia siku moja kabla ya kutimiza umri wa miaka 28, Februari 2008.
Hivyo, Sagna anawaonea huruma wachezaji wa Liverpool kutokana na kile kinachowakabili juu ya majonzi ya kumpoteza mchezaji mwenzao, Diogo Jota, mapema mwezi huu.
“Ikumbukwe nasi ni wanadamu,” alisema beki huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester City, akiongeza.
“Tunatumia muda mwingi kuwa na wachezaji wenzetu kuliko wake zetu na watoto wetu. Hivyo, hili litakuwa jambo gumu sana kwao. Sioni kama watacheza vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita.
“Kitu kigumu zaidi ni kumpoteza mpendwa wao. Siwaoni kabisa. Hii haitakuwa rahisi.”
Fowadi huyo wa Ureno, Jota na mdogo wake Andre walifariki dunia kwenye ajali ya gari kaskazini magharibi kwa Hispania, Julai 3.
Wachezaji wenzake wa Liverpool walishiriki kwenye maziko yake sasa amerejea kujiunga na timu kwa ajili ya mazoezi ya pre-season, huku wakiwa na kazi ya kutetea taji la Ligi Kuu England msimu ujao. Sagna anaamini wachezaji hao wanahitaji msaada mkubwa.
“Nilimpoteza kaka yangu 2008 wakati nipo Arsenal. Ulikuwa msimu wangu wa pili. Akili yangu ilipoteza kabisa, nilianza kufanya makosa mengi sana, makocha ya watoto wa shule. Kumiliki mpira ilikuwa tatizo,” alisema Sagna.