Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ATM YA WIKI: MR Bean anapiga hela bila kuongea

Muktasari:

  • Aliwahi kuwepo Charlie Chaplin, dunia ilivunjika mbavu kutokana na vichekesho vyake na kujizolea umaarufu kote duniani, lakini baada ya kufariki dunia mwaka 1977, hakuna aliyeamini atatokea mchekeshaji mwingine atakayeiteka dunia ya sanaa za vichekesho.

LONDON, ENGLAND: KWA kizazi cha miaka 2000, wanaweza wakawa hawazijui sana filamu za Rowan Sebastian Atkinson na jina lake maarufu ni Mr Bean kwenye sanaa za vichekesho duniani.

Aliwahi kuwepo Charlie Chaplin, dunia ilivunjika mbavu kutokana na vichekesho vyake na kujizolea umaarufu kote duniani, lakini baada ya kufariki dunia mwaka 1977, hakuna aliyeamini atatokea mchekeshaji mwingine atakayeiteka dunia ya sanaa za vichekesho.

Akaja 'Mr Bean', leo hii dunia inamkumbuka Chaplin huku ikiendelea kuburudika na Mr Bean, nani asiyemjua.

Kwa kutazama tu vichekesho vyake, unaweza ukaona ni mtu wa mizaha na hana maisha, lakini, kama hujui, ndiye mwigizaji wa vichekesho tajiri zaidi duniani.

Mr Bean amezaliwa na kukulia Consett, County Durham, England miaka 69 iliyopita na sifa kubwa katika uigizaji wake ni kuigiza pasipo kuzungumza na hata akizzungumza ni neno moja au mawili, lakini filamu zima ni vitendo tu na lazima utashika mbavu kwa kucheka.

Kwenye ATM leo, tutaangalia namna anavyotengeneza pesa ndefu na kuwa tajiri mkubwa huku akitajwa ni mmoja wa mastaa wanaoheshimika England na duniani.

ANAPIGAJE PESA

Chanzo chake kikuu cha mapato ni filamu alizoigiza na kuandika stori mwenyewe ambazo ni Blackadder, Mr Bean na Johnny English ambazo kwa pamoja zimeingiza zaidi ya Dola 1 bilioni, huku mwenyewe akichukua Dola 5 milioni.

Kijumla ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 150 milioni na mbali ya pesa za uigizaji pia ana madili ya ubalozi wa kampuni mbalimbali kama Kronenbourg na Fujifilm zinazomwingizia pesa.

Mbali ya filamu tajwa hapo juu, Rowan pia aliingiza pesa sana kupitia muvi yake ya Mr. Bean's Holiday ya mwaka 2007 ambayo ilizalisha zaidi ya Dola 229 milioni, huku Bean ya mwaka 1997 imezalisha Dola 250 milioni.


NDINGA

Kiujumla anakadiriwa kuwa na magari yenye thamani ya Dola 15 milioni na inaelezwa kuendesha magari yakifahari ni moja kati ya starehe yake.

Ndinga anazomiliki ni hizi-

1997 McLaren F1

2014 Bentley Mulsanne Birkin

Mercedes Benz SLS AMG

Rolls Royce Ghost

1986 Aston Martin V8 Zagato

 BMW 328 Roadster

2011 Rolls Royce Phantom Drophead

Land Rover Defender Heritage

Audi R8

Jaguar MK7


MJENGO

Kwa sasa anaishi England maeneo ya South Oxfordshire ambako anamiliki mjengo wenye thamani ya Dola 10 milioni.

Nyumba hiyo ina mandhari tulivu kama inavyoonekana kwenye picha na aliinunua mwaka 2006 kwa Pauni 2.5 milioni.

Eneo linalopatikana nyumba hiyo lina ukumbwa wa heka 16 ambazo zote zinamilikiwa na mchekeshaji huyu.

MSAADA KWA JAMII

Amekuwa mdau na balozi wa kampeni na mashirika mbalimbali ya kijamii ambayo yamejikita zaidi kwenye kusaidia watu wasiojiweza na mazingira kama Amnesty International, CAFOD, Charity Projects Entertainment Fund, Comic Relief, Global Goals, Kids Company, Prince's Trust, Save the Children na

UNICEF na kwa mwaka anatoa zaidi ya Dola 5 milioni.

MAISHA NA BATA

Alifunga ndoa na mrembo Sunetra Sastry, mwaka 1990, na hadi wanaachana mwaka 2015 walikuwa na watoto wawili.

Baada ya kuachana na Sunetra mwaka 2017, Rowan aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji mwenzake, Louise Ford ambaye hadi sasa wana mtoto mmoja.