Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico Madrid yavunja rekodi hizi, ikiichapa Barca

ATLETICO Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo ulikuwa una maana kubwa zaidi kwa Diego Simeone, kwani ulikuwa wa kwanza kwake kuupata kwenye uwanja wa Camp Nou tangu aanze kuifundisha Atletico.

BARCELONA, HISPANIA: BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Barcelona, Atletico Madrid imevunja rekodi mbili zilizokuwa zimedumu kwa muda mrefu.

Kikosi cha Diego Simeone kilikumbana na presha kubwa kipindi cha kwanza, lakini mambo yalibadilika dakika za mwisho kabla ya mapumziko baada ya Pau Cubarsi kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na faulo aliyomfanyia Julian Alvarez ambaye ndiye aliyefunga bao la kwanza kabla ya Alexander Sorloth aliyetokea benchi kuweka chuma chapili.

Alvarez alifunga bao la kuongoza kutokana na mpira wa adhabu uliotokana na tukio hilo na kuwapa wageni uongozi wa 1-0 kabla ya mapumziko.

Ushindi huo ulikuwa una maana kubwa zaidi kwa Diego Simeone, kwani ulikuwa wa kwanza kwake kuupata kwenye uwanja wa Camp Nou tangu aanze kuifundisha Atletico.

Kabla ya mechi hiyo, Barcelona ilikuwa haijapoteza hata mechi moja kati ya mechi 25 zilizopita dhidi ya Atletico kwenye uwanja huo katika mashindano yote.

Mara ya mwisho kupoteza ilikuwa Februari 2006, wakati Atletico ilipokuwa chini ya Pepe Murcia na ilichapwa mabao 3-1 katika mechi ya  La Liga.

Ushindi huo umevunja rekodi mbaya ya Atletico katika dimba hilo, pia umehitimisha mwendo mbaya waliokuwa nao ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya timu za Hispania.

Kabla ya hapo, Atletico hawakuwa wamewahi kushinda mechi ya ugenini dhidi ya timu ya La Liga kwenye mashindano hayo, wakipoteza mechi nne kati ya tano walizocheza.

Kwa sasa, ushindi huu umeiweka Atletico katika nafasi nzuri kuelekea mechi ya marudiano, itakayochezwa katika dimba lao la Wanda Metro Politano.

Katika mechi mbili za mtoano ilizowahi kucheza dhidi ya Barca, Atletico ilifanikiwa kusonga mbele mara zote ikiwa ni mwaka 2014 na 2016.