Atletico ikiwa siriazi inabeba huyu Alvarez

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya La Liga tayari imeshapeleka maombi kwa fowadi huyo wa kimataifa wa Argentina, ambaye huu ni msimu wake wa pili Etihad. Alvarez bado ni chaguo la pili kwenye nafasi ya mshambuliaji huko Etihad nyuma ya Erling Haaland, lakini sasa Atletico wanamtaka ili akakamatie nafasi ya kuwa mshambuliaji mkuu kwenye kikosi hicho.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA wa Manchester City, Julian Alvarez amefunguka na kuweka wazi kwamba yupo tayari kupokea ofa ya kwenda kujiunga na miamba ya soka ya Hispania, Atletico Madrid kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Miamba hiyo ya La Liga tayari imeshapeleka maombi kwa fowadi huyo wa kimataifa wa Argentina, ambaye huu ni msimu wake wa pili Etihad. Alvarez bado ni chaguo la pili kwenye nafasi ya mshambuliaji huko Etihad nyuma ya Erling Haaland, lakini sasa Atletico wanamtaka ili akakamatie nafasi ya kuwa mshambuliaji mkuu kwenye kikosi hicho.

Alvarez bado ana mkataba wa miaka minne kwenye kikosi cha Manchester City na kocha Pep Guardiola anafahamu wazi atapata namna nzuri ya kumtumia na kumpa dakika za kutosha ndani ya uwanja.  Fowadi huyo wa zamani wa River Plate alifunga mabao 19 na kuasisti mara 17 katika msimu wake wa kwanza. Na kwa mujibu wa Marca, Atletico inafahamu wazi kwenye mbio za kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa Argentina watachuana vikali na Barcelona. Atletico ina washambuliaji matata kabisa kama Antoine Griezmann, Memphis Depay na Alvaro Morata, lakini kocha Diego Simeone, anamtaka Muargentina huyo mwenzake akakipige Wanda Metropolitano.

Alvarez, 24, saini yake inaweza kugharimu pesa nyingi na hilo linaweza kumfanya abaki kwenye kikosi hicho cha Etihad, ambako mwenyewe amedai kwamba ameridhiwa na kiwango cha mechi alizochezeshwa msimu uliopita. Kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, Man City ipo kwenye hatari ya kuwapoteza mastaa wake wawili, De Bruyne na kipa Ederson.

PRE-SEASON

-Julai 23 v Celtic (Kenan Stadium, Chapel Hill, N.C.)

-Julai 27 v AC Milan (Yankee Stadium, New York)

-Julai 30 v Barcelona (Camping World Stadium, Orlando)

-Agosti 3 v Chelsea (Ohio Stadium, Columbus)