Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta awachana wachezaji Arsenal

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Ndoto ya Arsenal kutwaa mataji matatu ilizimika Jumamosi kwenye Uwanja wa St Mary's Stadium baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Southampton katika robo fainali ya Kombe la FA.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amewaambia wachezaji wake lazima wajifunze na kukabiliana na vipindi vigumu kuendana na hali ngumu vinginevyo  watajikuta wakimaliza msimu bila taji.

Ndoto ya Arsenal kutwaa mataji matatu ilizimika Jumamosi kwenye Uwanja wa St Mary's Stadium baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Southampton katika robo fainali ya Kombe la FA.

Ross Stewart aliifungia Southampton bao la kuongoza kabla ya Viktor Gyokeres kuisawazisha Arsenal baada ya kuingia akitokea benchi. Hata hivyo, Arsenal ilishindwa kushikilia bomba na ikaruhusu bao jingine dakika ya 85 kupitia Shea Charles.

Kwa matokeo hayo, Southampton imefuzu nusu fainali wakati Arsenal ikipata kipigo chao cha pili mfululizo baada ya awali kufungwa na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la Carabao kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Arteta alilazimika kupanga kikosi chenye wachezaji wapya kwa kiasi kikubwa kutokana na idadi kubwa ya mastaa wake ambao ni majeruhi.

Mambo yalionekana magumu kwake baada ya Gabriel Magalhaes kuumia kipindi cha pili, huku Arteta akisema moja ya sababu za kupoteza kwao ni hali mbaya ya hewa ya upepo mkali pamoja na majeruhi.

"Lazima uendane na hali halisi na ukabiliane nayo Ni lazima ujifunze kukabiliana na mazingira magumu katika mpira wa miguu ili kushinda taji, tunapaswa kuonyesha sisi ni nani. Tulikuwa na umiliki mkubwa wa mpira karibu na eneo la hatari. Tuliruhusu bao la kwanza kwa namna isiyo ya kawaida kwetu. Tulipata nafasi mbili kubwa ambazo tulipaswa kuzitumia. Ukifanya makosa ya kujilinda kama tulivyofanya leo, ni vigumu kufika nusu fainali."

Arsenal inatarajiwa kurejea uwanjani Jumanne, itakapokwenda Ureno kucheza dhidi ya Sporting Lisbon katika robo fainali ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya.