Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu Arsenal wajiondoa kambini

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Chama cha Soka England (FA), kimethibitisha kuwa Noni Madueke amepata majeraha na ameruhusiwa kurejea Arsenal kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuumia katika mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Uruguay.

LONDON, ENGLAND: UNAWEZA kusema ni gundu. Wakati Mikel Merino, Eberechi Eze, William Saliba, Gabriel Magalhaes, Leandro Trossard na Martin Odegaard wote wakiwa majeruhi, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amepata pigo lingine baada ya mastaa watatu kuripotiwa kupata majeraha na kuondolewa katika kambi ya timu ya taifa ya England.

Chama cha Soka England (FA), kimethibitisha kuwa Noni Madueke amepata majeraha na ameruhusiwa kurejea Arsenal kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuumia katika mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Uruguay.

Madueke na Adam Wharton ndio walioruhusiwa kuondoka mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini mbali na yeye, pia mastaa wengine wa Arsenal, Declan Rice na Bukayo Saka nao wamepewa ruhusa ya kuondoka kambini na kurudi haraka London kwa ajili ya matibabu zaidi, na hawatokuwepo katika mechi ijayo.

Badala yake, mastaa hao wawili wanarejea Kaskazini mwa London kujiunga na klabu yao inayowania ubingwa kwa ajili ya vipimo zaidi vya afya. Madueke, ambaye alianza mechi dhidi ya Uruguay akiwa amefungwa bandeji kwenye mkono wa kushoto, aliondoka katika dimba la Wembley akiwa amevaa kifaa maalum cha kusaidia goti baada ya kutoka nje ya uwanja akichechemea kabla ya mapumziko.

Hili linampa wasiwasi mkubwa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, ambaye yupo katika kipindi muhimu kinachohitaji timu yake kuwa kamili ili kupata matokeo na kutwaa ubingwa wa Premier League unaoonekana kuwa uko karibu yao zaidi.

Arsenal ilipoteza fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City kabla ya mapumziko ya timu za taifa, na mechi yao ya kwanza baada ya kalenda ya FIFA itakuwa ni robo fainali ya FA Cup dhidi ya Southampton Jumamosi ijayo. Kisha itacheza tena robo fainali ya kwanza ya UEFA Champions League dhidi ya Sporting CP nchini Ureno Jumanne.

Katika Ligi Kuu England, ambako kwa sasa inaongoza kwa pointi tisa, itacheza tena Aprili 11 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye dimba la Fly Emirates.

Hadi sasa haijajulikana Rice, Saka na Madueke watakaa nje kwa muda gani, na taarifa kamili inatarajiwa kutoka leo Jumatatu baada ya kufanyiwa vipimo zaidi.

Mastaa hao ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal kwa sasa, wakiwa wanatumika zaidi katika kikosi cha kwanza; hivyo, ikiwa watakosa baadhi ya mechi, inaonekana kuwa itakuwa pigo kubwa kwa Mikel Arteta. Tangu kuanza kwa msimu huu, Madueke amecheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao saba; Saka naye amecheza mechi 42 na kufunga mabao tisa, na Rice amecheza mechi 44 za michuano yote.